Viongozi wa dini,  Serikali na siasa nchini  wamehimiza umuhimu wa  kuendelea kumwombea dua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan ili aendelee kuwatumikia Watanzania  kwa haki, usawa na uadilifu ili kuharakisha upatikanaji wa Maendeleo ya kijamii na kiuchumi nchini.

Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir bin Ali, Naibu Waziri wa Mifugo Abdallah Ulega na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka, walieleza hayo  (jana)  Alkhamis 28 Aprili 2022 waliposhiriki katika  dua maalumu ya  kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe  Samia Suluhu Hassan  iliyofanyika katika msikiti wa Mtoro Jijini Dar Es Saalam.

Dua hiyo iliambatana na mkesha wa ibada ya usiku maalumu wa 'Lailatul al Qadir'  ilihudhuriwa na viongozi na waumini mbalimbali wa dini ya Kiislamu nchini.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...