MKURUGENZI wa mtandao wa kijamii wa Uturn Collection, Allen Salum Mhina (31), anayeishi Temeke, mtandao huo wa Uturn collection na Mange Kimambi App, wameshtakiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa makosa matatu likiwemo la kuchapisha maudhui yanayokiuka haki na uhuru wa mtu mwingine.

Mashtaka mengine waliyosomewa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Richard Kabate mwishoni mwa wiki iliyopita ni kufanya kazi ya uandishi wa habari bila kuwa na kibali na kutoka bodi ya ithibati ya wanahabari na kumfedhesha mtu kwa njia ya mtandao (cyber Bullying)

Hata hivyo upelelezi katika kesi hiyo namba 57 ya mwaka 2022 umeishakamilika na mshtakiwa Mhina anatarajiwa kusomewa maelezo ya awali (Preliminary Hearing) Aprili 27, 2022

Katika hati ya mashtaka iliyosomwa mahakamani hapo na mawakili wa serikali waandamizi Mwanaamina Kombakono akisaidiana na Sylivia Mitanto imedai Machi 9, 2022 katika maeneo tofauti ndani ya nje ya nchi ya Tanzania washtakiwa walichapisha video ya aliyekuwa Mbunge wa Mikumi, Joseph Haule maarufu kama Profesa Jay ambaye amelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kitengo cha wagonjwa Mahututi ( ICU) maudhui ambayo yanadhuru haki ya faragha ya mgonjwa (Profesa Jay)

Katika shtaka la pili inadaiwa kuwa katika tarehe tofauti kati ya Septemba 22,2022 na Machi 14,2022 huko Kinondoni eneo la Manyanya katika Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam mshtakiwa Allen na kampuni ya Uturn collection walifanya kazi ya uandishi wa habari bila ya kuwa na kibali kutoka bodi ya ithibati ya wanahabari.

Katika shtaka la tatu inadaiwa, Machi 9, 2022 katika maeneo tofauti ndani ya nje ya nchi ya Tanzania, mshtakiwa Allen kupitia mfumo wa kompyuta unaojulikana kama Mange Kimambi APP, unaosimamiwa na Uturn Colection alichapisha video ya aliyekuwa Mbunge wa Mikumi, Joseph Haule maarufu kama Profesa Jay ambaye amelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kitengo cha wagonjwa Mahututi ( ICU) kwa nia ya kusababisha emotional distress.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...