Na Khadija Kalili Kibaha
Wakongwe
wa siasa nchini Tanzania wamemzungumza na kummwagia sifa aliyekuwa
Rais wa Awamu ya Kwanza Hayati Julius Kambarege Nyerere ikiwa ni katika
kuadhimisha miaka 100 ya kuzaliwa kwake katika mdahalo uliofanyika
kwenye Shule ya Siasa ya Mwalimu Nyerere iliyopo Wilayani Kibaha Mkoa wa
Pwani.
Baadhi ya
viongozi waliodadavua sifa za Hayati Nyerere ni pamoja na Joseph Butiku
ambaye aliwahi kufanya kazi na Hayati Nyerere ambapo alisema kuwa
alikua ni mtu mwenye maadili na aliishia kwa utaratibu pia alipoanzisha
Chama Cha TANU aliweka utaratibu hivyo ni wajibu wa watu wote kuishi
katika misingi ya kuwa na utaratibu.
Mkongwe
Ally Mzee Ally kutoka Zanzibar alimwelezea Mwalimu Nyerere kuwa alikua
ni muumini wa umoja jambo ambalo alilitilia msisitizi mwaka 1957 ambapo
ndipo walupokutana na aliyekuwa Rais wa kwanza wa Zanzibar Hayati Abeid
Karume.
" kwa wakati huo alikua akiongoza Chama Cha
Afro Shiraz ambapo Mwalimu Nyerere alichangia sana kuleta ukombozi wa
Zanzibar hivyo wakafanya majadiliano na kukubaliana kuanzisha muungano
na kuunda nchi moja ya inayofahamika wa jina la Jamuhuri ya Muungano wa
Tanzania hivyo Kila mtanzania aelewe kuwa chimbuko la Muungano wa
Tanganyika na Zanzibar ulianza mwaka 1957"alisema Ally
Wakongwe
wengine waliozungumza ni pamoja na aliyewagi kuwa Waziri katika nyakati
tofauti pia Mbunge Mstaafu wa Jimbo la Bunda Stephen Wassira, wengine
waliozungumza ni pamoja na aliyewahi kuwa Katibu Mkuu Joseph Butiku
mstaafu ambaye alipata fursa ya kufanya kazi mbalimbali na Hayati
Nyerere alisema kuwa Mwalimu alikuwa mtenda haki ambaye alifundisha
watanzania kujitegemea na kujali utu wa kila mwananchi,pia alifundisha
ujamaa na kujitegemea binadamu wote ni sawa pamoja na kuandika Katiba
ya Chama,alikuwa mtu mwenye maadili na aliishi kwa utaratibu huku
alitaka watu wote watiitaratibu zote zilizowekwa.
"Amani
yetu tuilinde tuitunze tupinge ubaguzi ukabila ,udini tuwe wamoja
kwani hizi ndizo nguzo kuu za amani kwani endapo hizi hazitakuwepo basi
nchi haitakuwa na amani" alisema Ally.
Aliendelea
kwa kusema kuwa "Nimezungumza juu ya Imani ya Mwalimu Nyerere kuwa
viongozi hatuwezi kwenda mbele kama hatutafuata misingi ya haki kama
Katiba inachezwa itazaa rushwa, matapeli na machafu mengi yatazalishwa
hivyo nawashauri viongozi wa leo muachane na mambo ya ubaguzi kwani
Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ni nchi moja.
Kanali
Mstaafu wa Jeshi la Wananchi Tanzania Simba Kalia alimwelezea Mwalimu
Nyerere kuwa alikuwa na maoni katika nyanja ya uchumi Barani Afrika huku
akiwa na mani kwamba bila ya Afrika kuungana haitaendelea kwani Afrika
Ina kilakitu ikiwemo malighafi zote zinazogitajika katika kuitengeneza
bidhaa mbalimbali duniani.
"Mwalimu aliamini katika
kujenga uchumi wa viwanda Barani Afrika huku akiwa na maono ya kuwa
siku moja nchi yetu itakuwa nchi ya Viwanda huku utekelezwaji wake
ulianza kabla ya nchi kupata uhuru"alisema Kanali Mstaafu Simba Kalia.
Aliongeza
kwa kusema kuwa katika enzi zake za ujana alikuwa miongoni mwa vijana
waliopata mafunzo ya kiteknolojia katika nchi mbalimbali akiwa kama
mwanajeshi katika Shirika la Nyumbu lililoasisiwa na Mwalimu waliweza
kuunda vipuri vya magari ya aina mbalimbali.
"Mwalimu
ameondoka huku akiwa ameacha Taasisi na mifumo ambayo endapo
tutawarithisha vijana vijana taifa letu litakwenda mbele"alisema
Kanali Mstaafu Simba Kalia.
"Chini ya Uongozi wa
Mwalimu Nyerere alifanya mambo makubwa kwa taifa ikiwemo kuanzishwa kwa
kituo Cha Nyumbu,Mimi. nilikua mwizi mzuri sana wa teknolojia pia Niko
tayari endapo nitapatiwa fursa ya kuwafundisha vijana wetu hasa wale
wanaopita katika Jeshi la Kujenga Taifa JKT kwa sababu Nyumbu Kuna
karakana za kuitengeneza magari ikiwemo vipuri vya treni ya Mwendokasi
ambapo ujenzi wa reli yake unaendelea.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere Mzee Joseph Butiku akimvisha Katibu Mtendaji wa Chama Cha Mapinduzi Mstaafu na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Mstaafu Mzee Pius Msekwa (kulia) beji ya Maadhimisho ya Miaka 100 ya Mwalimu Julius Nyerere wakati wa Mdahalo wa Kitaifa wa kuadhimisha miaka 100 ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere uliofanyika katika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere, Kibaha mkoani Pwani leo Aprili 9, 2022. (Picha na Adam Mzee)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...