Na Humphrey Shao,Michuzi TV
Wito umetolewa Kwa Watanzania na Kenya kuongeza mahusiano ya kitaaluma bila kuangalia tofauti zao za Mipaka ya nchi zilizomo katika jumuiya ya Afrika Mashariki.
Wito huo umetolewa hivi Karibuni na Naibu Mkuu wa Tasisi ya Teknolojia ya Dar es Salaam (DIT) ,Prof Patrick Nsimama wakati wa hafla ya kuwaaga wanafunzi 24 waliokuja kujifunza katika Chuo hicho kupitia mradi wa RAFIC.
Prof. Nsimama ametaja kuwa licha ya nchi zetu kutenganishwa na Mipaka lakini Bado ni Moja Kwa maana ya Jumuiya na Bara Zima la Afrika.
"DIT Ndio Sehemu pekee ambayo kinajengwa kituo Cha umahiri Kwa ajili ya ICT Kwa ukanda huu wa Afrika Mashariki, hivyo ni vyema Vijana na watumishi waliopo katika jumuiya kuja Tanzania kuchota maarifa yaliopo katika kituo hicho" Amesema Prof.Nsimama.
Aidha Amesema licha ya kuwa tofauti ya Mipaka Bado wanafunzi wetu wameonesha kuwa mitaala ya ufundishwaji hayatofautiani baina ya nchi na nchi, ndio maana wanafunzi hawa 24 kutoka Kenya wamefanya vizuri katika mafunzo yao.
Amesema wanafunzi hao wamjifunza Masuala ya Graphics Disigner ,Animation na Masuala ya Mtandao.
Mratibu Radical na Mradi wa RAFIC ,Dr.Joseph Matiko akizungumza umuhimu wa mradi huo
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...