Wasanii mbalimbali wa Bongo Muvi wanatarajia kukutana katika hoteli ya serena jijini dar es salaam hivi karibuni,kwa ajili ya maandalizi makubwa ya kumpokea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe,Samia Suluhu Hassan ambaye kwa sasa yuko nchini Marekani kwa ajili ya ziara ya uzinduzi wa Filamu ya Royal Tour nchini Marekani.


Akiwa nchini Marekani,Rais Samia alipata nafasi  ya kuwasemea Wasanii wa Bongo Muvi na kujaribu kuwatafutia nafasi/fursa za kufika mbali kupitia tasnia hiyo adhimu hapa nchini.

Kufuatia kitendo hicho cha Rais Samia kuwakumbuka Wasanii hao,kimewafurahisha na kuwavutia Wasanii hao na kuamini kuwa Rais Samia anatambua mchango wao na yuko pamoja nao katika kuhakikisha anawasaidia kwa namna ama nyingine ili waweze kusogea zaidi katika tasnia hiyo ambayo imekuwa ikiajiri vijana wengi kila kukicha.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...