Na Khadija Khamis –Maelezo

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ikishirikiana na Taasisi Binafsi imeandaa maonesho ya kibiashara yanayotarajiwa kufanyika Maisara Mjini Zanzibar, ikiwa ni Shamramra ya  kuelekea  Maadhimisho ya miaka 58 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Maonesho haya yanatarajiwa kuanza tarehe 22 april hadi tarehe 6 mei ambapo Makamu wa Rais wa  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Phillip Mpango anatarajiwa kuzinduwa maonyesho hayo.

Akitoa taarifa kwa waandishi wa Habari huko Baraza la Wawakilishi Chukwani , Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais (Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi ) Mhe. Hamza Hassan Juma amesema harakati za ujenzi wa miunombinu ya maonesho hayo inaendelea katika viwanja vya Maisara .

Amesema jumla ya Shilingi milioni 250 zinatarajiwa kutumika katika maadhimisho hayo ambazo zitatolewa na wafanya biashara ambao watashiriki katika maonyesho hayo.

Aidha alisema Sherehe za Maadhimisho hayo zitaanza kwa Kongamano ambalo linatarajiwa kufanyika tarehe 20 mwezi huu katika Ukumbi wa Gorden Tulip, Uwanja wa Ndege Zanzibar na Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa ni Makamu wa Pili wa Rais Mheshimiwa  Hemed Suleiman Abdulla.

Alifafanua kuwa  Kongamano hilo litazungumzia suala zima la Muungano ikiwemo mafanikio na changamoto pamoja na kuelezea historia za Waasisi wa Muungano huo.

Mhe. Hamza Ametoa wito kwa Wananchi kujitokeza kwa wingi katika maonyesho hayo licha ya kupata  fursa za Biashara pia watapata ufafanuzi wa taarifa  mbalimbali za muungano.

 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais (Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi )  Mhe.Hamza Hassan Juma akitoa taarifa kwa  waandishi wa Habari kuhusu maadhimisho ya miaka 58 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar huko Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Chukwani Zanzibar.

PICHA NA FAUZIA MUSSA –MAELEZO ZANZIBAR.




 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...