WAZIRI wa Kilimo Mhe.Hussein Bashe amekutana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Interlinked Group International Dkt. Yasser Mansour.
Dkt. Mansour ameambatana na Bw. Salah Bamatraf na Marafiki zao kutoka Iran.
Katika mazungumzo yao Dkt. Mansour amemueleza Mhe. Waziri nia yao ya kuwekeza kununua mazao ya nafaka kama vile Ngano, Mahindi, Mchele, Soya na Vyakula vya Mifugo kwa ajili ya kuunza nje ya nchi.
Aidha Dkt. Mansour amesema watawekeza kwenye ununuzi wa matunda kama vile maembe, mananasi na ndizi na kusafirisha nje ya nchi.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...