Mkuu
wa mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge, ametembelea Mradi wa barabara ya
kiwango cha Zege Kwala-Vigwaza inayounganisha katika mradi mkubwa wa
Kimkakati wa Bandari kavu Kwala yenye urefu wa km.15.5 ambao utagharimu
sh.bilioni 36 na umefikia asilimia 54.1.
Barabara
hii inapunguza athari zitokanazo na kupitisha malori mazito kwenye
barabara ambazo hupelekea matengenezo ya barabara kuwa na gharama kubwa
kila wakati,ni mkombozi kwa vijiji vya Vigwaza,Mnindi na Kwala na
itarahisisha shughuli za uchukuzi kati ya bandari na barabara Kuu ya
Morogoro.
Akitembelea
mradi huo pamoja na kujionea Hali ya ujenzi bandari kavu ya Kwala ,
Kunenge alieleza ,Ni ziara inayojibu maelekezo waliyopewa na Katibu
kiongozi wiki kadhaa zilizopita wakati alipofika eneo hilo na kuwataka
kuhakikisha ndani ya miezi mitatu barabara na bandari hiyo iwe imeanza
kazi.
"Mradi huu
unakwenda katika maeneo makubwa ya uwekezaji Kongani ambayo itajengwa
viwanda 300-350 ,Bandari Kavu, maeneo ya kubadilisha vichwa vya treni":
"Tunampongeza
na kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan,aliahidi kutekeleza na kumaliza
miradi iliyoanza tangu kipindi cha awamu ya tano na kuanzisha miradi
mipya Kama huo wa Kongani ya uwekezaji wa viwanda":alisema Kunenge.
Kunenge
alielekeza ,miezi mitatu barabara ya zege na bandari iwe imekamilika na
kuanza kutoa huduma.:;"- ,Lakini tunafahamu pia itaendelezwa kujengwa
barabara nyingine ya njia mbili ":Kazi yetu Ni kusimamia na kuhakikisha
miradi hii inajengwa kwa viwango vinavyotakiwa na kukamilika kwa wakati
kwa manufaa ya wananchi na Taifa."
"Ni
eneo la kimkakati, wenzetu wa Burundi,Uganda,Rwanda watakuwa na eneo la
kuhifadhi mizigo Yao ,Ni eneo linalozunguka viwanda watakuwa
wanasafirisha mizigo Yao,tutakuwa na reli SGR, barabara, EPZA."
Mkuu
huyo wa mkoa alibainisha wapo nyuma ya Rais kusimamia miradi yote ,na
eneo la uwekezaji ambapo ametembea falme za Kiarabu,Dubai,Ufaransa,
Marekani kutafuta wawekezaji na kuitangaza nchi matarajio yetu kupata
wawekezaji wengi na mkoa upo vizuri .
Awali
msimamizi wa mradi wa barabara hiyo, Jacob Mambo alisema , mradi
ulianza Novemba 2020, Mamlaka ya Bandari (TPA) ilimpatia Wakala wa
barabara Tanzania TANROADS jukumu la kusimamia ujenzi wa barabara hii
Kama Mhandisi Mshauri kupitia kitengo Cha TECU Mkoa wa Pwani.
Alifafanua,
matabaka ya chini yameshafikia zaidi ya asilimia 90 ya kazi,Tabaka
lililoimarishwa kwa saruji limejengwa kwa asilimia 81.29 ,makaravati ya
kupitisha maji asilimia 96.3 na madaraja makubwa matatu kwa asilimia
100.
Mambo alieleza
,Tabaka la zege limefikia asilimia 40 ambapo jumla ya mradi umefikia
asilimia 54.1 na utakamilika baada ya miezi miwili na nusu.
Alisema
kulikuwa na changamoto ndogondogo lakini Serikali na TPA wameshamaliza
,na mkandarasi kishalipwa asilimia 33 na mradi ni wa Bilioni 36.
Kwa
upande wake Alexander Ndibalema kutoka TPA ,alieleza kati ya heka 502
,wameshazungusha uzio heka 60 una urefu wa km.2.96 ,heka 5
wameziendeleza kwa Ajili ya Bandari na kazi imefanywa na SumaJkt .
Ndibalema
alisema ujenzi unaenda Sambamba na ujenzi wa barabara kwa Ajili ya
uingizaji mizigo, mizigo itakayofika bandari ya Kwala itakuwa inakwenda
kwa njia ya reli ,na ujenzi umefikia asilimia 65 na utakamilika kwa
miezi miwili na nusu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...