Na Farida Said, Morogoro.

Wakala wa Usajili  wa Biashara na Leseni (BRELA), imeibuka mshindi wa pili kati ya taasisi 15 za Serikali zilizoshiriki kutoa huduma kwenye maonesho ya Tano ya  Mifuko ya Programu za Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, mkoani Morogoro.

 Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo ya ushindi wa pili na  Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), jana tarehe 14 Mei, 2022, Afisa Mtendaji Mkuu wa  BRELA Bw. Godfrey Nyaisa amesema, ushindi huo umetokana na huduma ambazo maafisa wa BRELA wamekuwa wakizitoa kwa wananchi  wa Manispaaa ya Morogoro wakati wote wa maonesho.

Bw. Nyaisa amesema wakati wote wa maonesho wananchi wamefurika kwa wingi katika banda la BRELA kupata elimu na kurasimisha biashara zao huku wengi wakikamilisha usajili wa majina ya biashara na kutoka na cheti cha usajili papo kwa papo.

 Bw. Nyaisa amewasihi wafanyabiashara kutumia mfumo wa  usajili kwa njia ya mtandao kurasimisha biashara zao kwani huduma hiyo kwa sasa ni rahisi na inamuwezesha muombaji kupata huduma bila kufika katika ofisi za taasisi hiyo.
 
Bw. Nyaisa ameongeza kuwa    BRELA inajivunia ushindi huo kwani imeyatumia vyema  maonesho hayo kwa kutoa huduma na kuongeza kuwa;
“Sisi hapa hatukuja kufanya maonesho sisi tumekuja kufanya kazi ndio maana unaona wafanyakazi wote hapa wamekuja na vitendea kazi vyao, hivyo mwananchi akifika banda la BRELA anapata majibu ya maswali yake yote pamoja na ushauri,” amefafanua Bw.Nyaisa.

Aidha Bw. Nyaisa amesema kuwa mfumo uliopo sasa wa urasimishaji  biashara ni rahisi na rafiki zaidi kwa waombaji wote walio mjini na vijijini, hivyo ametoa wito kwa wafanyabiashara kuacha tabia ya kuwatumia  "vishoka" kurasimisha  biashara zao.

“ Kwa sasa  mfanyabiashara  hutakiwi kufika kwenye ofisi za zetu, unaweza kupata huduma ukiwa hata sebuleni kwako na ukapata cheti bila ya usumbufu wowote,”amesisitiza Bw. Nyaisa.

Taasisi iliyoshinda nafasi ya kwanza katika maonesho hayo yaliyohitimishwa jana ni Shirika la Posta Tanzania, huku Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) ikichukua nafasi ya tatu.




 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...