Na Janeth Raphael - Bungeni Dodoma


Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania DKt.Tulia Ackson amesema kwa sasa hawezi kutamka kuwa viti 19 vya wabunge wa chama cha Demokrasia n nna Maendeleo (CHADEMA) waliofukuzwa uanachama vipo wazi, kwa kuwa suala hilo lipo mahakamani.

DKt. Tulia ameliambia bunge jijini Dodoma kuwa kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mamlaka yenye kauli ya mwisho ya utoaji haki ni mahakama.

Amesema kwa kuwa tayari alipokea barua kutoka kwa wabunge hao 19 wakimtaarifu kuwa tayari wamefungua shauri mahakamani kupinga kufukuzwa uanachama, Bunge haliwezi kuingilia mchakato wa mahakama na badala yake linalazimika kusubiri hadi hapo mahakama itakapotoa uamuzi wake.

Spika amesema Alipokea Barua za Wabunge hao zikieleza kuwa Maamuzi hayo si halali, ni kinyume, hayakuzingatia haki ya msingi ya kuwasikiliza, kujitetea
Wabunge hao wamefungua Rufaa Mahakamani ya Kupinga Maamuzi hayo
Afisa wa Chadema alitumwa kupeleka Barua kwa Spika wa Bunge na kisha kuambiwa asubiri lakini alipokea simu kutoka kwa Viongozi wa Chadema wakimtaka aondoke eneo hilo na hivyo watafanya utaratibu mwingine wa kuituma Barua hiyo.

“Ninalazimika kutotangaza kwamba nafasi 19 za Wabunge wa Viti maalum wa Chadema hazitabaki wazi mpaka pale mahakama itakapotoa maamuzi, Kama kutakuwa na swali lolote Msemaji wa Mwisho wa jambo hii ni Spika wa Bunge na si yeyote” Spika wa Bunge Dkt. Tulia

Tarehe 12 mwezi huu Baraza Kuu la CHADEMA lilitupilia mbali rufaa ya wabunge hao ambao walikuwa wakipinga kufukuzwa uanachama na Kamati Kuu ya chama hicho, na hivyo kumlazimu Katibu Mkuu wa CHADEMA John Mnyika kuwasilisha barua kwa Spika kumtaarifu kuhusu jambo hilo ili aendelee na taratibu nyingine.

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...