Na Mwandishi wetu, Simanjiro
WAJUMBE wa Halmashauri Kuu ya CCM ya Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, wamempongeza Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuandaa filamu ya Royal Tour ambayo itasaidia kuchochea utalii nchini.
Wajumbe hao wa Halmashauri ya Wilaya hiyo wametoa azimio hilo walipokutana kwenye kikao hicho kilichofanyika mji mdogo wa Orkesumet ambayo ni makao makuu ya Wilaya ya Simanjiro.
Katibu wa CCM Wilaya ya Simanjiro, Amos Shimba amesema kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya hiyo kwa kauli moja wanampongeza Rais Samia kwa kufanikisha Royal Tour ambayo itaongeza watalii nchini.
Shimba amesema Royal Tour imezidi kuitangaza nchi kimataifa hivyo kufaidika na idadi kubwa ya watalii ambao watafika wengi zaidi na fedha za kigeni kuongezeka.
Mbunge wa Jimbo la Simanjiro, Christopher Ole Sendeka amesema Rais Samia wanampongeza na kumshukuru Rais Samia kwa kuzidi kuitangaza Tanzania katika ngazi ya kimataifa.
"Kupitia mapato yatakayopatikana kupitia wageni watakaokuja nchini baada ya kuiona Royal Tour tunatarajia kupata madarasa ya shule za msingi na sekondari, zahanati, vituo afya na huduma za maji," amesema Ole Sendeka.
Katibu wa UWT Wilaya ya Simanjiro, Leokadia Fisso amesema kupitia filamu ya Royal Tour vivutio vingi nchini vitapata watalii wengi hivyo kuongeza pato la Taifa nchini.
"Hifadhi zetu za Taifa za Tarangire na Manyara nazo kwa kiasi kikubwa zitafaidika kupitia filamu hii ambayo muhusika mkuu ni mama yetu Rais Samia kwani watalii wataongezeka," amesema Fisoo.
Diwani wa Kata ya Loiborsiret Ezekiel Lesenga Mardad amesema Rais Samia ameionyesha dunia kuwa Tanzania ina vivutio vingi vya utalii.
Mjumbe wa kikao hicho kutoka Kata ya Mirerani, Jack Momo amesema wanamshukuru Rais Samia kwa kutoa kazi nzuri ya filamu ya Royal Tour itakayoongeza idadi ya watalii nchini.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...