Picha: Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Zainab Chaula akiwa kwenye picha ya pamoja na Wawakilishi wa Mradi wa USAID Afya Yangu akiwemo Mkurugenzi Mradi Dkt. Marina Njelekela (kulia) na Meneja Mradi Nyantito Machota (kulia nyuma) walipofika ofisini kwake jijini Dodoma kujitambulisha wengine ni Wakurugenzi kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wanawake na Makundi Maaalum
Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Zainab Chaula amekutana na wadau kutoka Mradi wa USAID Afya Yangu kenye Ofisi za Wizara jijini Dodoma.
Ujumbe kutoka Mradi wa USAID Afya Yangu uliongozwa na
Mkurugenzi wa Mradi Dkt. Marina Njelekela na Meneja Mradi Nyantito Machota.
Katika kikao hicho Dkt. Zainab Chaula na Wawakilishi wa Mradi wa USAID Afya Yangu wamejadiliana mambo kadhaa ikiwepo uwezeshaji wa Wanawake kiuchumi na masuala ya Kijinsia.
Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum inaendelea kukutana na wadau mbalimbali ili kuhakikisha inaweka mikakati na Mipango ya kuwahudumia wananchi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)




Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...