Na Mwamvua Mwinyi,Pwani

MWENGE wa Uhuru umetembelea Jumla ya miradi 15 yenye thamani ya sh. milioni 967.821.5 katika wilaya ya Mafia na kupitisha miradi yote.

Kati ya miradi hiyo miradi mitatu imezinduliwa, nane imetembelewa minne imewekwa jiwe la msingi .

Akikabidhi mwenge wa Uhuru Kisarawe mkuu wa wilaya ya Mafia Mhandisi Martin Ntemo, alisema Serikali Kuu imetoa zaidi ya milioni 900,
Halmashauri 19.1 michango ya uhuru milioni 10 na wananchi 2.290 .

Ntemo alishukuru miradi yote imepitishwa na kudai kwamba mafanikio ya Mafia ni ya mkoa hivyo ushirikiano uliopo ndio utakaofikisha maendeleo zaidi kwa mkoa huo kwa kushindanishwa na mikoa mingine.

Kabla ya makabidhiano ya mwenge Mafia na Kisarawe katika viwanja vya ndege ,uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere , kiongozi wa mbio za mwenge Kitaifa Sahir Geraruma aliwapongeza Mafia kwa usimamizi mzuri wa miradi ya maendeleo kinachotakiwa kifanywe na wilaya zote na mikoa mingine.

Alisema Mafia inapaswa iendelee kujengwa Ni kisiwa kizuri ,licha ya Mazingira Ni magumu Lakini viongozi wanafanya kazi nzuri ,endeleeni na juhudi hizo kuunga mkono Serikali katika suala zima la kusukuma gurudumu la maendeleo.

Vilevile Geraruma aliwataka viongozi wasichoke kukumbusha wananchi ujumbe wa mbio za mwenge mwaka huu ,ikiwemo Kujitokeza katika Zoezi la sensa agost mwaka huu, mapambano dhidi ya malaria,rushwa , utumiaji wa madawa ya kulevya na kupambana na maambukizi mapya ya VVU.

Akipokea mwenge huo kutoka Mafia, Mei 5 mwaka 2022 ,Mkuu wa wilaya ya Kisarawe Nickson Saimon ,alisema Miradi yote Ina thamani ya Bilioni moja , milioni Mia Tisa arobaini ,elfu mia mbili themanini na mbili ,Mia nane tisini na nane na Senti thelathini na moja (1,940,282,898.31).

Nickson alieleza Kati ya fedha hizo Serikali Kuu 717,392,124.76, Halmashauri 10,000,000, Wananchi 705,858,431.76,wahisani 502,032,341.79 na michango ya mwenge 5,000,000.

"Vijiji 21 kati ya 65 wilayani humo ,urefu wa km.192.99 pia mwenge huu utapitia miradi Nane ambapo mradi mmoja utawekewa jiwe la msingi,miradi minne itazinduliwa na miradi mitatu itatembelewa na kukaguliwa "alifafanua Nickson.

Mkuu huyo wa wilaya aliongeza, miradi itakayopitiwa imegusa sekta za Elimu ,afya,maji , barabara,uwezeshaji wananchi kiuchumi na uzalishaji mali na mifugo.

Mwenge huo unatarajia kuingia wilaya ya Kibaha Mei 6 na Mei 7 mwaka huu .


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...