Naibu Ofisi yaWaziri Mkuu, Sera Bunge na Uratibu Mhe. Ummy Nderiananga amepongeza Halmashauri ya Jiji la Tanga kwa kupunguza kiwango cha maambukizi ya virusi vya ukimwi kutoka 3.5% mwaka 2020 hadi kufikia 3.2% kwa mwaka 2021.

“Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwenye bajeti Mpya ya serikali 2022-2023 itakayoanza mwezi wa saba ameongeza fedha eneo kutoka Billion 1 Mpaka Billion 1.8”

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri Ofisi yaWaziri Mkuu, Sera Bunge na Uratibu Mhe. Ummy Nderiananga alipokuwa akipokea taarifa ya Mkoa wa Tanga ya Mapambano dhidi ya virusi vya Ukimwi.

Aidha Naibu Waziri Mhe. Ummy Nderiananga ameshauri Halmashauri za wilaya kuona umuhimu wa kutenga fedha za Mapambano Dhidi ya Virusi vya Ukimwi. Hii itasaidia kuwawezesha katika miradi ya vikundi vya watu wanaoishi na virusi vya ukimwi (WAVIU) kufanya shughuli zao za maendeleo vizuri.

Wananchi msiogobe kujitokeza kupima virusi vya ukimwi, mpime mjitambue afya zenu. Kama Kauli mbiu inavyosema pima VVU, Jitambue ishi alisema Naibu Waziri Ummy

“Mabinti mnao toa elimu rika, endeeleni kuwaelimisha mabinti wenzetu. Asilimia kubwa ya maambukizi ya virusi vya ukimwi yapo kwa vijana na asilimia 80% ya hao vijana ni mabinti lazima tuendele kuelimishana, Naibu waziri Ummy”

Naye Naibu katibu Mkuu Bwn. Kaspar Mmuya amesema Baraza la Watu Waoishi na Virusi Vya Ukimwi ambao wamejitokeza na kujitangaza na kusema wako tayari kushirikiana na serikali kutoa elimu (NACOPHA) ni baraza muhimu.

“Hili baraza ni rasilimali kubwa sana kufikia malengo yetu, wanaishi kwa mfano na wanamalengo na wanatusaidia hata wale walioachaa dawa kwa sababu mbalimbali wanawatafuta na kuongea nao na kuwarudisha kwenye dawa alisema, Naibu Katibu Mmuya”

Ninaomba hizi afua mbalimbali za ukimwi zinazofanyika, maelekezo yatoke mradi wowote unahusu mambo ya ukimwi washirikiane na NACOPHA. Hawa wanauwezo wa kufikia walengwa mpaka ndani kijijini na wanatusaidia kufikia malengo ya taifa kwa kutumia muda vizuri na fedha vizuri. 


Naibu Waziri Ofisi yaWaziri Mkuu, Sera Bunge na Uratibu Mhe. Ummy Nderiananga akizungumza na viongozi na watendaji wa Mkoa wa Tanga alipokuwa akipokea taarifa ya Mkoa huo ya Mapambano dhidi ya Virusi vya Ukimwi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...