Na John Walter-Manyara
Kamati ya Mpango kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto ( MTAKUWA)za vijiji na mitaa zimetakiwa kupambana na vitendo vya ukatili vinavyofanywa katika maeneo yao ili kupunguza tatizo hilo katika Mkoa wa Manyara unaotajwa kuongoza kwa vitendo hivyo.
Wito huo umetolewa na Nemence Mabung'ai mdau wa kupinga masuala ya Ukatili kutoka shirika lisilo la serikali la wakati wa maadhimisho ya siku ya Uhuru wa vyombo vya habari iliyofanyika mjini Babati.
Naye Kaimu afisa maendeleo ya jamii ustawi Mkoa wa Manyara Lilian Bujune amesema Mkoa wa Manyara unaongoza kwa vitendo vya kikatili ambapo kimkoa inashika nafasi ya pili na ukeketaji nafasi ya kwanza hali inayoleta taswira mbaya katika Mkoa huu.
UKATILI
Amewaitaka jamii hasa waandishi wa habari kupaza sauti na kutoa elimu kwa jamii ili kuepukana na vitendo vya ukatili ambapo amesema vitendo vingi vya ukatili vinaanzia katika ngazi za familia.
Afisa huyo amesema Mkoa huo unatajwa kuwa miongoni mwa inayoongoza kwa unyanyasaji, huku vitendo vilivyokithiri zaidi ikiwa ni ubakaji, vipigo na ulawiti wa watoto wadogo.
“Hali ya ukeketaji kitaifa ni asilimia 10, kimkoa Manyara ni asilimia 58 ya wanawake bado wanafanyiwa ukatili huo, ukatili mwingine ni wanawake kuzalisha mali, lakini kwenye matumizi hawahusiki hata ardhi hawaruhusiwi kumiliki,” alisema.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...