Na John Walter-Manyara

Jamii imetakiwa kutumia mitandao ya kijamii kwa manufaa ya maendeleo binafsi na taifa kwa ujumla.

Wito huo umetolewa na Maarufu Mkwaya wakati akifungua maadhimisho ya Uhuru wa vyombo vya habari Mkoa wa Manyara yaliyoandaliwa na klabu ya Waandishi wa Habari mkoani hapa Mei 9,2022.

Mkwaya amesema kupitia mitandao ya kijamii mtu anaweza kufanya Biashara ya kuuza au kununua,kutangaza vivutio mbalimbali kwa faida ya Taifa kuliko kuchapisha Mambo yasiyo na maadili mema kwenye jamii.

Amesema wapo baadhi ya watu wasio waaminifu wasiozingatia matumizi sahihi ya mitandao hiyo na kusababisha upotoshaji kwa wanaotumia mitandao hiyo kwa ajili ya kujifunza na kuhabarika.

Maadhimisho ya Uhuru wa vyombo vya habari hufanyika kila Mei 3 ya kila mwaka ambapo kitaifa yalifanyika jijini Arusha na kuhudhuriwa na Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.

Miongoni mwa mada zinazojadiliwa katika maadhimisho hayo, ni pamoja na uandishi wa habari na changamoto za kidijitali, matumizi ya teknolojia na usalama mtandaoni.Kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu ni uandishi wa habari na changamoto za kidijitali.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...