Kampuni ya usafiri kwa njia ya mtandao nchini Bolt imesema itandelea na huduma za usafiri nchini kama kawaida.
Kufuatia taarifa iliyochapishwa tarehe 20 Aprili, 2022 na mtandao wa TechCrunch, yenye taarifa yetu (Bolt) kuhusu hali ya biashara nchini Tanzania kama matokeo ya AGIZO jipya NA. LATRA/01 12022 la tarehe 14 Machi 2022, Bolt Tanzania imekuwa na mkutano wenye mafanikio na LATRA tarehe 27 Aprili, 2022 ili kujadili zaidi suala hili.
Akizungumza kuhusu taarifa hiyo Meneja wa Bolt kanda ya Afrika Mashariki Kenneth Micah amesema "Kutokana na mkutano tuliofanya, tunapenda kueleza kwamba tumepiga hatua kubwa katika kufikia suluhu la jambo hili na tunatarajia utatuzi wa haraka".
Aliendelea kusema "Bolt inapenda kusisitiza kwamba imejitolea kuendelea kutoa huduma za usafiri kwa soko la Tanzania, na kutengeneza fursa za ujasiriamali zinazowezesha watu wengi zaidi kujikimu kimaisha".
Bolt bado ina matumaini kuwa ushirikiano wetu na washikadau husika ikiwa ni pamoja na LATRA utatoa mapitio mazuri ya kanuni kuhusu ushuru, na uwekaji kamisheni kwa makampuni ya vyombo vya usafiri wa kukodi ili kuwezesha shughuli endelevu za kazi zetu, alimaliza kusema Micah.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...