Na Amiri
Kilagalila,Njombe
Kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 121
kimefanikisha ununuzi wa gari jipya aina ya land cruser hard top kwa
ajili ya utoaji huduma za kichungaji katika parokia ya Utalingolo jimbo
katoliki la Njombe kutokana na kuwapo kwa changamoto ya uhaba wa vyombo vya
usafiri.
Taarifa ya makabidhiano ya gari hilo katika
kanisa hilo iliyosomwa na katibu mkuu wa kamati ya uhamasishaji wa
ununuzi wa gari hilo bwana Deogratias Mtewele imesema fedha hizo zimetokana na
michango mbalimbali ya waumini,wadau wa maendeleo pamoja na wafadhili toka nje
ya nchi.
“Kamati ya ununuzi wa gari ya parokia iliundwa
mwaka 2019 mwezi septemba,na imeafanikiwa kununua hii gari mpya yenye tahamani
ya shilingi milioni 121 laki tatu elfu 57 na 666 amabpo fedha hizo zilitokana
na michango ya waumini na wafadhili wa ndani nan je ya nchi”alisema Deogratias
Mtewele
Mwenyekiti wa kamati ya uhamasishaji wa ununuzi
wa gari hilo bwana Erasto Mpete ambaye ni makamu mwenyekiti wa halmashauri ya
mji wa Njombe na diwani wa kata ya Utalingolo anasema haikuwa kazi rahisi
kupatikana kwa chombo hicho cha usafiri .
“Gari hili litumike kwa ajili ya uinjilishaji na
kumtukuza Mungu tuombe chombo hiki kitunzwe ili kiweze kutumika kwa muda mrefu”alisema
Mpete
Kwa niaba ya mbunge wa jimbo la Njombe mjini
Deodatus Mwanyika katibu wa mbunge huyo Andreas Mahali anasema ushirikiano wa
pamoja ndio unaowafikisha mbali wananchi kimaendeleo kama walivyoshirikiana
kununua gari hilo.
Mwanasheria wa mkoa wa Njombe Hilmar Danda
akimwakilisha mkuu wa mkoa anasema ni lazima serikali iendelee kuziunga mkono
dini zote licha ya kuwa yenyewe haina dini.
“Lazima tufanye kazi kama timu ili tuweze
kufanikiwa,tuepukane na ile ya kusema mimi nitafanya na tuseme sisi tutafanya
na ndio maana Utalingolo leo hii mnafurahia matokeo hayo”alisema Mahali
Padre Athanas Mgimba kwa niaba ya askofu
jimbo katoliki la Njombe anasema kila muumini wa kanisa katoliki Utalingolo
anapaswa kuwa mlinzi wa gari hilo huku paroko wa parokia hiyo padre lukas mgaya
ameshukuru jitihada zilizofanyika hadi kupatikana kwa gari hilo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...