KATIBU Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Daniel Chongolo amewasili mkoani Simiyu huku akipokewa na Viongozi wa CCM Wilaya na Mkoa na Viongozi wa Serikali wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo Mhe.David Kafulila.

Ndugu Chongolo amepokewa njia panda katika Kata ya Isanga wilaya ya Maswa katika Jimbo la Maswa Magharibi, Simiyu leo Mei 31,2022 akitokea mkoani Shinyanga

Ndugu Daniel Chongolo ambae pia ni Mlezi wa Mkoa huo ameanza ziara ya kikazi katika Mkoa wa Simiyu, ambapo pamoja na mambo mengine ni kuimarisha na kuhimiza uhai wa chama kuanzia ngazi ya mashina.

Chongolo ambaye ameambatana na Mjumbe wa Kamati Kuu na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Ngemela Lubinga pia atazungumza na wanachama wa Chama hicho pamoja na kukagua miradi ya maendeleo kama ilivyoahidiwa kwenye Ilani ya uchgauzi Mkuu mwaka 2020-2025.














Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...