Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Daniel Chongolo akipanda ngazi kukagua mradi wa ujenzi wa tenki la maji lenye ujazo wa lita Laki tano katika kijiji cha Mwakitolya, Shinyanga Vijijini leo Mei 29,2022 mkoani Shinyanga.
Tenki hilo ambalo tayari limeishakamilika linatarajia kuhudumia Wananchi zaidi ya 14,000. Mradi huo unafadhiliwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa gharama zaidi ya shilingi Milioni 364.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Daniel Chongolo akikagua mradi wa ujenzi wa tenki la maji lenye ujazo wa lita Laki tano katika kijiji cha Mwakitolya,Shinyanga Vijijini leo Mei 29,2022 mkoani Shinyanga.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Daniel Chongolo(Wa kwanza kushoto) kutoka kwa  Mkurugenzi Mtendaji wa  KASHWASA,Mhandisi Patrick Nzamba(wa kwanza kulia) kuhusu  mradi wa ujenzi wa tenki la maji lenye ujazo wa lita Laki tano katika kijiji cha Mwakitolya,Shinyanga Vijijini leo Mei 29,2022 mkoani Shinyanga.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji KASHWASA Mhandisi Patrick Nzamba (kushoto) mara baada ya kukagua ujenzi wa tanki la maji Mwakitolwa unaogharimu zaidi ya shilingi za Kitanzania milioni 364,ikiwa sehemu ya ziara yake ya kukagua utekelezwaji wa ilani ya uchaguzi ya mwaka 2020-2025 mkoani Shinyanga.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akisalimiana na Katibu wa Shina namba 9 Tawi la Mwakitolya Ndugu Amos Yohana (kulia) alipowasili kusalimia na kuzungumza na wakati wa shina hilo, ikiwa sehemu ya ziara yake ya kukagua utekelezwaji wa ilani ya uchaguzi ya mwaka 2020-2025 mkoani Shinyanga
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akipandisha bendera ya Chama katika shina namba 9 kuashiria uzinduzi wa shina hilo, ikiwa sehemu ya ziara yake ya kukagua utekelezwaji wa ilani ya uchaguzi ya mwaka 2020-2025 mkoani Shinyanga

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akisalimiana na Mwenyekiti wa Shina namba 9 Tawi la Mwakitolya Mzee Ali Matembele (kulia) alipowasili kusalimia na kuzungumza na wakati wa shina hilo, ikiwa sehemu ya ziara yake ya kukagua utekelezwaji wa ilani ya uchaguzi ya mwaka 2020-2025 mkoani Shinyanga.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...