Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine amekutana na kufanya mazungumzo na Mjumbe Maalum wa Serikali ya Jamhuri ya Czech Balozi Miloslav Machalek katika mazungumzo yaliyofanyika katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam.
Mjumbe huyo maalum wa Serikali ya Czech Balozi Machalek amewasilisha andiko la Serikali ya nchi hiyo la kutaka kushirikiana na Tanzania katika maeneo ya usimamizi wa maji, kilimo, afya, ICT na biashara.
Akizungumza katika kikao hicho Balozi Sokoine ameongelea kufurahishwa na wazo la kuihusisha Tanzania katika mradi huo ambao alisema kuwa utaimarisha uhusiano na ushirikiano kati ya Tanzania na Jamhuri ya Czech.
Balozi Machalek amesema andiko aliloliwaasilisha katika kikao hiko ni mradi wa maendeleo ambao nchi yake unakusudia kuutekeleza katika nchi tano za Afrika za Tanzania, Tunisia, Kenya, Ghana na Ivory Coast.
Balozi Machalek aliambatana na Balozi wa Jamhuri ya Czech nchini Tanzania mwenye makazi yake nchini Kenya Mhe. Martin Klepetko ambaye pia alitumia fursa hiyo kuzungumza na Balzoi Sokoine katika kuimarisha uhusiano na ushirikiano kati ya Tanzania na Jamhuri ya Czech.
Naye Balozi wa Jamhuri ya Czech ameelezea nia ya Serikali ya Czech kushirikiana zaidi na Tanzania kupitia Nyanja za biashara na uwekezaji ili kukuza ushusiano na ushirikiano kwa faida ya pande zote mbili na kuongeza kuwa ni matumaini yake kuwa uhusiano mzuri ulipo baina ya nchi hizo utaendelea kuimarika.
Katibu
Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi
Joseph Sokoine akipokea ujumbe kutoka kwa Mjumbe Maalum wa Serikali ya
Jamhuri ya Czech Balozi Miloslav Machalek alipokutana naye katika ofisi
ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam tarehe 06 Mei, 2022.
Katibu
Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi
Joseph Sokoine akimsikiliza Balozi wa Jamhuri ya Czech mwenye makazi
yake nchini Kenya Mhe. Martin Klepetko (katikati) walipokutana katika
ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam tarehe 06 Mei, 2022 wakati
Mjumbe Maalum wa Serikali ya Jamhuri ya Czech Balozi Miloslav Machalek
(kushoto) alipowasilisha ujumbe wake kwa Katibu Mkuu.
Katibu
Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi
Joseph Sokoine akizungumza na Balozi wa Jamhuri ya Czech mwenye makazi
yake nchini Kenya Mhe. Martin Klepetko walipokutana katika ofisi ndogo
za Wizara jijini Dar es Salaam tarehe 06 Mei, 2022.
Katibu
Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi
Joseph Sokoine akizungumza na Balozi wa Jamhuri ya Czech mwenye makazi
yake nchini Kenya Mhe. Martin Klepetko (katikati) walipokutana katika
ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam tarehe 06 Mei, 2022. Pembeni
ya Balozi Sokoine ni Mkurugenzi wa Idara ya Amerika na Ulaya Wizara ya
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Swahiba Mndeme
akiwa na afisa dawati Bi Agness Kiama.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...