MKURUGENZI wa kiwanda cha
Animal Care co.Ltd , Mlandizi,Kibaha Mkoani Pwani ,Dkt Salaa Hamdun
amesema endapo Serikali itaendelea kutatua changamoto ya wafugaji katika
usimamizi wa kupata soko la uhakika kwenye maziwa na bidhaa za mifugo
pamoja na kuweka Bei elekezi itasaidia kuongeza kipato Chao.
Akizungumza
namna wanavyosaidiana na jamii inayowazunguka na Wafugaji , Mkurugenzi
wa kiwanda hicho kinachozalisha vyakula vya mifugo na virutubisho
alisema, bei bado ni ndogo kwa bidhaa za mifugo ukilinganisha na Gharama
za vyakula ambazo zinapanda huku bei ya kuku sokoni ikiendelea kumbana
mfugaji na mkulima moja kwa moja.
"Suala
Kama Hilo Ni kusema Serikali isaidie wafugaji kuweza kusimamia masoko
Yao na kucontrol bei maana bei ya maziwa , bidhaa za mifugo bado
ndogo";"; alifafanua Hamdun.
Hamdun
alieleza kwamba, kiukweli wafugaji wanapata Faida ndogo na wakati
mwingine kupata hasara kubwa hivyo sekta ya kilimo kupitia Serikali ni
vyema ikatupia macho suala hili ili kupunguza makali ya kimaisha kwa
kundi la wafugaji.
Vilevile
alishukuru Serikali kwa kuendelea kusimamia wawekezaji na changamoto
zinazowakabili hasa kutatua kero ya umeme,maji na baadhi ya miundombinu.
Alisema,kiwanda
cha Animal Care sasa kinazalisha vyakula vya mifugo na virutubisho Tani
2,500 kwa mwezi na kutoa ajira 200 za moja kwa moja.
Hamdun
alielezea , wanatumia
malighafi za kitanzania kwa asilimia 90,"Tuna mchango ndani ya jamii inayotuzunguka ,na jamii, wafugaji wanamchango kwetu tukiwa kama wawekezaji.
malighafi za kitanzania kwa asilimia 90,"Tuna mchango ndani ya jamii inayotuzunguka ,na jamii, wafugaji wanamchango kwetu tukiwa kama wawekezaji.
Alisema, licha ya hayo Lakini malighafi nyingine kama soya,mahindi wanapata Zambia na Malawi Jambo ambalo ni changamoto kwao.
Aliomba
wafugaji kukimbilia fursa ya kutumia kiwanda hicho kurahisisha kupata
soko huku changamoto zao zikiendelea kufanyiwa kazi.
Awali
mkuu wa wilaya ya Kibaha Sara Msafiri,alisema wilaya inaendelea
kushirikiana na wawekezaji pamoja na wafugaji kutatua changamoto
zinazowakabili ili kuinua maendeleo ya sekta ya Mifugo na kukuza uchumi.
Kiwanda
hicho Ni moja ya viwanda ambavyo vimetembelewa na mwenge wa uhuru
Mkoani Pwani na kuhimiza wawekezaji kutoa ajira hasa kwa wazawa ,
kushirikiana kwa maendeleo ndani ya jamii na kulipa Kodi ili kuongeza
Pato la Taifa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...