Watumishi wa Mamlaka ya Usafiri Ardhini (LATRA) leo Mei mosi wameungana na  watumishi wengine kusherehekea siku ya wafanyakazi duniani (Mei Mosi) ambayo Kitaifa imefanyika Dodoma na Dar es Salaam yakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla katika Uwanja wa Uhuru uliopo Temeke  jini Dar es Salaam.

Watumishi watatu kutoka LATRA ambao ni Bw. Philipo Ngongi, Bi. Habiba Chambali pamoja na Bw. Thomas Matope   wametunukiwa utumishi bora na kupongezwa na Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam Amos Makalla.

Maadhimisho ya mwaka huu yamebebwa na Kaulimbiu isemayo "Mishahara na Maslahi Bora kwa Wafanyakazi Ndio Kilio Chetu. Kazi Iendelee".
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla akimpongeza Mfanyakazi wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)  Philipo Ngongi  mara baada ya kutangazwa kuwa mfanyakazi Bora kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani mwaka 2022 yaliyofanyika kimkoa katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
Wafanyakazi wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) wakiwa kwenye maandamano kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani mwaka 2022 yaliyofanyika katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam
Wafanyakazi Bora wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)  wa kwanza kushoto ni Thomas Matope, kati ni Habisa Chambali na kulia ni Philipo Ngongi wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada kutangazwa kuwa wafanyakazi Bora kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani mwaka 2022 yaliyofanyika katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
Wafanyakazi Bora wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)  wakiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi pamoja na wafanyakazi wenzao wa LATRA mara baada ya kutangazwa kuwa wafanyakazi Bora kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani ambayo yamefanyika katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
Wafanyakazi wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) wakiwa Uwanja wa Uhuru wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani mwaka 2022 yenye Kaulimbiu isemayo "Mishahara na Maslahi Bora kwa Wafanyakazi Ndio Kilio Chetu. Kazi Iendelee"
Wafanyakazi wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani mwaka 2022 yaliyofanyika katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
Gari la Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) likipita kwenye maandamano ya Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani mwaka 2022 yenye Kaulimbiu isemayo "Mishahara na Maslahi Bora kwa Wafanyakazi Ndio Kilio Chetu. Kazi Iendelee" yaliyofanyika katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...