Na Karama Kenyunko, Michuzi TV

MTENDAJI Mkuu wa Mahakama, Profesa Elisante Ole Gabriel amesema wamejipanga kupunguza idadi kubwa ya makosa yanayofunguliwa mahakamani kwa kutoa elimu kwa watanzania mubashara, kwani watapoelimisha jamii hakutakuwa na sababu ya kwenda mahakamani.

Profesa Gabriel amesema hayo leo Mei 19, 2022 wakati akizungumza na waandishi wa habari, juu ya masuala ya kutoa taarifa mubashara na kutaja mashirika ambayo wameingia nayo mikataba katika ushirikiano wa kupeana taarifa.

Amesema wamegundua katika mnyororo wa haki, elimu kwa umma ndiyo inayotakiwa, ambapo katika tafakari na tasmini zao wameona itapunguza wananchi kufunguliana mashauri yasiyokuwa na sababu za msingi.

"Elimu hii itasaidia watanzania kushirikiana na kuacha tamaduni za kufungua mashauari mahakamani, lakini wanatakiwa kukaa kwa pamoja na kuyamaliza na ndiyo maana tumeaandaa mada ili wananchi waweze kuuliza maswali na kujibiwa," amesema.

Profesa Gabriel, amesema program hiyo imeanza kupitia ITV na TBC, ambapo kadri ya mafungu yanavyoruhusu wataendelea kuwa mubashara pia katika vyombo vingine vya habari.

Profesa  Gabriel, amesema mwaka mmoja (wiki 52), ambapo kila mwezi itakuwa anazungumza yeye kwa kuzungumzia mada zitakazotolewa.
Amesema kwa sasa wana mada za wiki nne, mada ya kwanza ambayo tayari imeishatolewa na ITV ambayo ni maboresho ndani ya Mahakama, mada ya pili ni usimamizi wa mirathi na kutatua changamoto zake.

Amesema mada ya wiki ya tatu itakuwa kuelekea matumizi ya tehema na kupunguza karatasi na ya nne ni uboreshaji wa miundombinu.

"Tunaomba wananchi wafuatilie ili wajifunze na kisha ametoa rai kwa wazazi, walezi na walimu kuwa ni wakati wa wakuruhusu watoto na wanafunzi kujifunza kwenye  mlolongo wa haki na sio kuangalia katuni, wakifundihswa maadili itakuwa ni jambo jema sana.

Akizungumzia wadau ambao wameshaingia nao mikataba katika kushirikiana kwa kupeana taarifa ni Ofisi ya Mkurugenzi  wa Mashtaka nchini, NIDA, Kituo cha Sheria na Vitendo, Brela,Rita, Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

"Kutokana na ushirikiano huu hii tutafikia malengo yetu yenye ubora na utoaji haki waraka kwa sababu tutakuwa inaokoa muda na pia nitoe wito kwa wananchi watoe taarifa na ushahidi wa uhakika, kwa sababu Mahakama inafanya kazi kwa weledi na umakini,"amesema.

Pia amewataka wananchi wasiishie kulalamika bali watoe taarifa zao ili zifanyiwe kazi, ambapo wanaweza kutumia namba 0752 500400 kwa ajili ya kutoa malalamiko  yao kwa masaa 24.

Mtendaji Mkuu wa Mahakama Prof. Elisante Ole Gabriel akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mabadiliko ya mifumo ya kimahakama ilivyojipanga kurusha vipindi mbalimbali vya kutoa  elimu kwa wananchi namna ya kujua haki zao za msingi za kisheria pamoja na wao kuuliza maswali kupitia vipindi hivyo vitakavyokuwa vikirushwa kupitia televisheni ya Taifa ya Tbc na ITV Mbashara leo Mei 19,2022 jijini Dar es Salaam

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...