MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango leo tarehe 20 Mei 2022 anatarajiwa kuondoka nchini kuelekea Davos nchini Uswisi ambapo atamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Jukwaa la Uchumi Duniani (World Economic Forum) unaotarajiwa kufanyika tarehe 22 hadi tarehe 26 Mei 2022.

Katika mkutano huo, Makamu wa Rais atahudhuria mikutano mbalimbali inayohusu masuala ya biashara na uwekezaji, ulinzi na usalama, usalama wa chakula, mazingira pamoja na mabadiliko ya tabia ya nchi.

Mkutano wa Jukwaa la Uchumi Duniani unahudhuriwa na Wakuu wa Nchi na Serikali kutoka mataifa mbalimbali, Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa, Wakuu wa Taasisi na Makampuni mbalimbali duniani pamoja na Wafanyabiashara.

Franco Singaile
Msaidizi wa Makamu wa Rais - Habari

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...