Na Said Mwishehe Michuzi TV-Ruangwa
KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Shaka Hamdu Shaka amepokelewa na mamia ya maelfu ya Wanachama na Wananchi wa Wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi.
Shaka amewasili kwenye Wilaya hiyo akitokea katika Wilaya za Lindi Mjini na Lindi Vijijini ambapo amekuwa akiendelea na ziara ya ukaguzi wa utekelezaji wa Miradi ya maendeleo pamoja na kuangalia Uhai wa Chama hicho.
Katibu huyo wa Itikadi na Uenezi wa CCM alipookea katika eneo la Mandawa ambapo baada ya kuwasili shangwe kutoka kwa Wananchi waliokuwepo kwenye eneo hilo liliibuka huku baadhi ya akina mama walishindwa kuficha furaha zao kiasi cha kuamua kugalagala chini.
Katika eneo hilo la mapokezi Wananchi walipata nafasi ya kutoa shukrani zao kwa Shaka ambaye amefika kwenye Wilaya yao kwa ajili ya kushuhudia kazi kubwa na nzuri inayoendelea kufanywa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Uongozi mahiri wa Rais Samia Suluhu Hassan.
Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi Hassan Ngoma ametumia nafasi hiyo kumueleza Shaka kwamba Wananchi wa Wilaya hiyo wameridhika na kazi inayofanywa na Rais Samia ya kuleta maendeleo kwenye nyanja mbalimbali."Katika Wilaya yetu tunashukuru Rais Samia, ameendelea kutuletea maendeleo, kwetu tunasema hatuna deni naye, Mama ameendelea kuupiga mwingi sana.
"Katika Uchagauzi Mkuu wa mwaka 2025 tunasema Rais Samia asiwe na wasiwasi, Wananchi wa huku tumeshaamua kura zote ni za kwake.Rais Samia Samia ameongeza fedha za maendeleo kwenye Wilaya yetu,hivyo miradi ya maendeleo inaendelea kila Kona,"amesema Ngoma.
Wakati huo huo Shaka akiwa kwenye mapokezi hayo ameendelea kuwakikishia Wananchi kuwa Serikali ya CCM itaendelea kuwa kimbili na suluhisho la changamoto kwa kuzitafutia ufumbuzi hatua kwa hatua."Tunafahamu kuna kazi kubwa na nzuri inayoendelea kufanywa na Rais Samia Suluhu Hassan.Wananchi wenyewe tangu nimeingia Mkoa wa Lindi na leo niko hapa Ruangwa wanakiri Rais amekuwa chachu ya maendeleo ndani ya Mkoa huo."
Baada ya mapokezi hayo Shaka na msafara wake amepata nafasi ya kutembelea miradi na kukagua ujenzi inayoendelea kwenye miradi hiyo ikiwemo ya ujenzi wa vituo vya Afya, miradi ya maji safi na salama, miradi ya ujenzi katika sekta ya elimu pamoja na kuzungumza na wananchi.

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka akipiga Ngoma ya. ligongo baada ya kupokelewa na kushiriki ujenzi wa jengo la Zahanati ya Kijiji cha Chikundi, Kata ya Chikundi alipowasili wilayani Ruangwa, Mkoa wa Lindi kwa ziara ya kikazi kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM na Uhai wa Chama.

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka akizungumza na wana CCM katika Kijiji cha Mandawa wilayani Ruangwa, Mkoa wa Lindi akiwa katika ziara ya kikazi kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM na Uhai wa Chama mkoani Lindi.

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka akicheza na vijana wa hamasa baada ya kupokelewa katika Kijiji Cha Mandawa, Kata ya Mandawa alipowasili wilayani Ruangwa, Mkoa wa Lindi kwa ziara ya kikazi kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM na Uhai wa Chama.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...