Na Said Mwishehe, Michuzi TV-Ruangwa


USHIRIKI wa Wananchi wa Wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi katika shughuli za maendeleo, umemfurahisha Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Shaka Hamdu Shaka, hivyo amesema umefika wakati kwa Watanzania kushiriki kikamilifu kwenye ujenzi wa Taifa.

Shaka amesema Rais Samia Suluhu Hassan sasa ameirejesha ari ya wananchi kwenye maeneo mbalimbali kushiriki ujenzi wa miradi ya maendeleo unaakisi zama za ujamaa na kujitegemea za Chama Cha Mapinduzi kama ilivyoasisiwa na viongozi wa taifa wakiongozwa na hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere na hayati Sheikh Abeid Amani Karume.

Akizungumza mbele ya maelfu ya wananchi pamoja na wanachama wa CCM Shaka ambaye yupo kwenye ziara ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchgauzi ya CCM ya mwaka 2020/2025, Shaka amesema kujitolea kwenye maendeleo ni jambo linalopaswa kupewa kipaumbele na kila mwananchi na utaratibu huo uwe kwa wote.

"Mwenye kokoto, mwenye simenti, mwenye kila kitu tunakwenda kuunga nguvu ujenzi wa taifa ili kufikia maendeleo kwani hatuna mjomba, hatuna shangazi, hatuna mama mdogo atakayetoka anakotoka aje atufanyie kazi ya kujenga maendeleo kwa umoja wetu, mchango wetu ni muhimu ili Chama hiki kuhakikisha kimesimama.

"Wazee wetu walifanya haya tunayoyafanya sisi (kujitolea nguvu). Nimefarijika sana na kinamama mnavyotisha katika kushika hatamu za kuongoza nchi kama ambavyo Rais Samia anafanya, lakini mnatisha kwenye kuhamasisha maendeleo.

"Wakinamama kwenye ujenzi wamekuwa wengi zaidi, kwenye uhamasishaji wamekuwa wengi zaidi, kwenye kutuongoza wanafanya vizuri zaidi kama anavyofanya Rais Samia, Mungu awabariki sana, Mungu awalinde sana mama zetu kwa namna ambavyo mnaleta ari na shime kwenye taifa hili," anasema.

Awali akizungumza kwa nyakati na maeneo tofauti baada ya kupokeleewa na wananchi katika Kijiji cha Mandawa, wilayani humo, Shaka amesema serikali chini ya Rais Samia itaendelea kuleta maendeleo kwa kasi.

Shaka amesema kutokana na kutambua mchango wa wakulima serikali ya awamu ya sita itaendelea kutatua changamoto za wananchi na anatambua huko nyuma kulikuwa na changamoto katika kilimo cha zao la korosho, lakini serikali chini ya Rais Samia imeendelea kuzitafia ufumbuzi.

Kwa mujibu wa Shaka, miongoni mwa utatuzi wa changamoto ni pamoja na kutoa ruzuku ya pembejeo kwa wakulima wa korosho ambazo zitagawiwa bure kwa wakulima wa zao hilo.







Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...