Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh Anthony Mavunde ametangaza leo kuanzisha mashindano makubwa ya Ndondo Cup Jijini Dodoma kwa kushirikiana na muandaaji wa Ndondo Cup Bw. Shaffih Dauda.
Mbunge Mavunde ameyasema hayo leo wakati akifunga mashindano ya MAVUNDE CUP ya Chuo cha Serikali za Mitaa-Kampasi ya Mjini yaliyofanyika leo katika uwanja wa Jamhuri Dodoma.
“Ninawapongeza kwa ubunifu huu wa kuanzisha mashindano ya michezo mbalimbali ya ndani ya Chuo,ninaahidi kuwaunga tena mkono katika mashindano ya mwakani.
Lakini pia mjiandae na mtengeneze Timu moja yenye nguvu ishiriki katika mashindano ya NDONDO CUP ambayo natarajia kuyaanzisha pamoja na Bw. Shaffih Dauda hapo Dodoma kwa lengo la kuibua vipaji na kuendeleza Michezo jijini Dodoma”Alisema Mavunde
Akishukuru kwa niaba,Mkuu wa Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo Dr. Mpamila Madale amemshukuru Mbunge Mavunde kwa ufadhili wa mashindano hayo ya michezo kwa wanachuo na kumuomba kuendelea kushirikiana na uongozi wa chuo katika kuendeleza michezo Chuoni hapo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...