Na Mwandishi Wetu
MSHINDI wa Tsh. Bilioni 1.2 ya Jackpot ya Sportpesa, Florian Valerian Massawe amesema kuwa katika kubashiri michezo 13 ya Jackpot, alipata shida kupata matokeo ya mchezo mmoja wa Villarreal dhidi Real Sociedad ambao walikuwa wageni wa mchezo huo, Sociedad walipata ushindi wa bao 2-1.

Akizungumza wakati akikabidhiwa mfano wa hundi ya kiasi hicho cha pesa jijini Dar es Salaam, Florian amesema kuwa alipata shida kupata matokeo ya mchezo huo ambao ulikuwa wa mwisho kukamilisha mkeka wake wa mechi 13.

“Mpaka dakika 67 ya mchezo, timu hizo zilikuwa 1-1, nilimuita Mke wangu (Mama Dennis) aje aangalie kwanza! baada ya kuona matokeo hayo nilikuwa na wasiwasi sana, nilienda kuangalia baadae Sociedad walipata bao la pili, nilikuwa siamini kabisa kama kweli nimeshinda”, amesema Florian.

Kwa upande wa Mke wa Mshindi huyo, Lightness Florian amesema alikuwa anaona huruma kwa mumewe kutoa kiasi kikubwa cha pesa katika Kubashiri michezo hiyo ya bahati nasibu, amesema siku ambayo alishinda kiasi hicho cha pesa (Tsh. Bilioni 1.2) ilikuwa furaha na heka heka ndani ya nyumba yao.

“Aliniita kwa sauti ya ukali sana, sikujua nini kinaendelea siku hiyo, kumbe ilikuwa anafuatilia mchezo huo ambao ulimpa ushindi na kukamilisha ubashiri wa michezo yote 13”, amesema Lightness.

Naye Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi SportPesa, Tarimba Abbas alitoa pongezi kwa Florian kwa ushindi wake na kuwa Bilionea wa kwanza aliyetokana na kubashiri mpira wa miguu nchini Tanzania.

“Kwa bahati nzuri mshindi wetu amepatikana wakati tunasherehekea miaka 5 tangu kuanza shughuli hizi za michezo ya kubashiri hapa nchini Tanzania. Ushindi wa Florian umefanikisha dhamira yetu ya kuwawezesha na kuwainua watanzania kiuchumi na kutengeneza bilionea wa kwanza”, amesema Tarimba.

Akizungumza kwa niaba ya TRA Mkuu wa Kitengo cha Michezo ya Kubahatisha, Shabani Mwanga amempongeza Florian kwa ushindi alioupata wa zaidi ya Bilioni 1 na pia kama Mtanzania mzalendo amechangia kwenye uchumi wa nchi kwa kodi ya Tzs 188,297,109 ambayo imetokana na ushindi wake wa Jackpot.
JP winner 8 4- Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi SportPesa Tarimba Abbas , Mkurugenzi Mtendai Bodi ya michezo ya kubahatisha James Mbalwe, Mkuu wa kitengo cha michezo ya kubahatisha Shabani Mwanga wakimkabidhi mshindi wa Sportpesa Jackpot ya Tsh. 125,316,060 Florian Valerian Massawe.
JP winner 8 3- Mshindi wa Jackpot ya SportPesa Florian VAlerian Massawe akikabidhiwa rasmi mfano wa hundi ya Tsh. 1,255,316,060 na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi SportPesa Tarimba Abbas.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...