Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe. Mhamed Omary Mchengerwa kushoto akisaini mkataba mkataba wa makubaliano ya kusaidiana katika kuboresha maeneo ya Sekta anazozisimamia kulia ni Balozi wa China nchini Wang Ke kwa upande wa Serikali ya watu wa China kwenye Ofisi ya Ubalozi wa China jijini Dar es Salaam





Na John Mapepele.


Serikali ya Tanzania na China leo, Mei 26, 2022 zimetiliana Saini mkataba wa makubaliano ya kusaidiana katika kuboresha maeneo ya Sekta anazozisimamia.


Utiaji wa Saini wa mikataba hiyo ya kihitoria umeongozwa na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe. Mhamed Omary Mchengerwa kwa upande wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Balozi wa China nchini Wang Ke kwa upande wa Serikali ya watu wa China kwenye Ofisi ya Ubalozi wa China jijini Dar es Salaam.

Akizungumzia kuhusiana na manufaa ya mikataba hiyo, Mhe. Mchengerwa amesema Serikali ya Tanzania imesaini mikataba hiyo ya ushirikiano inatarajia kuleta mapinduzi makubwa kwenye sekta hizo.

Amesema kwa upande wa utamaduni kutakuwa na kupeleka wadau wa utamaduni, sanaa na michezo katika nchi ya china na watu wa china kuja nchini kwa ajili ya kubadilishana uzoefu.

Kwa upande wa elimu Tanzania itapeleka wanafunzi ambapo China itafadhili masomo haya kwa kutoa nafasi 120 kwenda kwenye maeneo ya lugha, utamaduni, sanaa na maeneo mengine ya hinsia (humanities) kila mwaka ambapo Tanzania itatoa ufadhili wa nafasi 15 kwa ajili ya wachina kuja Tanzania kusoma hasa kwenye maeneo ya hinsia(humanities) pamoja na maeneo ya lugha.

Aidha, amesema mkataba huu unatarajiwa kutoa nafasi kwa wataalam kwenye maeneo ya sekta hizo zote. Pia imeelezwa kuwa Serikali ya China inatarajia kujenga vituo vya kisasa vyenye miundombinu yenye viwango vya kimataifa vya sanaa na utamaduni ambavyo vitatumika na wasanii wa hapa nchini katika kuzalisha kazi zao zenye ubora ambazo zitauzwa duniani.


“Ni jambo la kumshukuru Mwenyezi Mungu kuwa wasanii wetu wanakwenda kupata studio za kisasa kabisa kwa ajili ya kuzalisha kazi zao”amefafanua Mhe. Mchengerwa.

Aidha, amesema Tanzania inaamini kuwa Tanzania imebarikiwa kuwa na utamaduni uliosheheni vitu vingi kutokana na kuwa na makabila ambayo ni zaidi ya 120.

Amesema kulingana na mikataba hiyo Serikali za nchi zote zinakusudia kuchangamsha utamaduni na sanaa ili ziwe kwenye kiwango halisi tofauti na sasa ambapo inaonekana kuwa kutochangamka kwa kiwango hicho.

Katika ziara hiyo Waziri Mchengerwa ameambatana na Katibu Mkuu wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Dkt, Hassan Abbasi na Wakurugenzi wa Sekta za Utamaduni na Sanaa kwenye Wizara hiyo, ambapo kwa Serikali ya China Mhe. Balozi Wang Ke ameambatana na watendaji waandamizi kwenye sekta hizo.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...