Na Mwamvua Mwinyi, Chalinze


MKUU wa wilaya ya Bagamoyo, Zainab Abdallah ameeleza miradi 25 yenye thamani ya Bilioni 47.2 inapitiwa na Mwenge wa Uhuru kati ya miradi hiyo ni pamoja na kuweka jiwe la msingi mradi wa kipekee wa Ufugaji Afrika Mashariki na Ukanda wa Sahara .

Akipokea mbio za Mwenge wa Uhuru ukitokea wilaya ya Kibaha, huko Ruvu Darajani alieleza wilaya hiyo ina Halmashauri mbili ambapo Halmashauri ya Chalinze itatembelewa miradi 14 iliyogharimu milioni 937.8 na Bagamoyo miradi 11 yenye thamani ya Bilioni 46.3.

Aidha alimshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwapatia Bilioni 1.6 fedha za Uviko Chalinze na kujenga madarasa na miradi 66 ya shule za Sekondari .

Mkuu huyo wa wilaya alieleza kwamba, kwa Halmashauri ya Bagamoyo imepokea Bilioni 1.02 na kujenga shule shikizi 14 na Sekondari 37.

"Tunamuahidi Rais Samia kuwa hatutamuangusha ,katuteua kumsaidia kazi na hapa kwetu Chalinze na Bagamoyo tunapiga kazi ili kuleta maendeleo"alisema Zainab.

Zainab alifafanua, wilaya hiyo inategemea zaidi chanzo Cha mapato ya ndani Cha kokoto na mawe ambayo yanapelekwa jijini Dar es Salaam na maeneo jirani.

"Asilimia 60 ya mapato ya ndani yanatokana kwenye kokoto na mawe, ndio maana sisi miradi yetu ipo vizuri kwakuwa tunatumia malighafi inayotoka kwetu wenyewe "alisisitiza Zainab.

Vilevile akizungumzia suala la sensa ya watu na makazi alieleza, Zoezi la anwani na makazi wameshalitekeleza kwa asilimia 100 Hadi Sasa.

Mbunge Wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete alisema ushauri, mapungufu wanayopatiwa watayafanyia kazi ili baadae miradi iwe Bora kwa maslahi mapana ya wananchi wa Chalinze.

Kiongozi wa mbio za mwenge Kitaifa Sahir Geraruma alihimiza usimamizi makini wa miradi kwani Serikali inatumia fedha nyingi hivyo inatarajia matokeo chanya yenye tija kwa Watanzania.

Miradi iliyopitiwa Chalinze ni pamoja na kuona shughuli za usafirishaji abiria -pikipiki ambao umegharimu milioni 41.8 kati ya fedha hiyo mil.32.6 Ni mkopo wa asilimia 4 ya vijana kutoka Halmashauri na milioni 9.2 Ni fedha ya wanakikundi  na kuweka jiwe la msingi ujenzi wa jengo la wodi ya mama na mtoto pamoja na upasuaji kwa fedha ya tozo.

Pia kuzindua mradi wa ukarabati wa barabara Pingo, kufungua vyumba viwili vya Madarasa na ugawaji wa vifaa vya ujenzi vinavyotokana na asilimia 5 ya mchango ya mwenge, kufungua kituo cha afya Sekondari Imperial, mradi wa kisima Kibiki na kuzindua ujenzi wa madarasa manne ya uviko19

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...