NA FARIDA SAID MOROGORO.

Mkemia Mkuu wa Serikali Daktari Fidelis Mafumiko ameionya jamii kuepuka ununuzi na matumizi holela ya dawa zisozosajiliwa wala kuthibitishwa na mamlaka husika ikiwemo kuangalia aina za viambata au kemikali zilizotumika katika kutengeneza dawa hizo.

Amelisema matumizi holela ya dawa yanaweza kumsababisha mtu kupata madhara ya kiafya kutokana na kushindwa kufahamu aina ya kemikali zilizotumika kutengeneza dawa hizo.

Dk Mafumiko amewataka wananchi kununua dawa zilizothibitishwa na mamlaka husika kwa kuwa ni halali kwa matumizi ya biaadamu au wanyama.

Dk. Mafumiko ameyasema hayo alipotembea banda la Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali katika maonesho ya tano ya mifuko na programu za uwezeshaji wananchi kiuchumi yaliofanyika katika viwanja vya Jamuhuri mkoani Morogoro.

Aidha amewataka wajasiriamli wakubwa,wadogo pamoja na wananchi kwa ujumla kutumia fursa ya maonesho mbalimbali yanayoandaliwa na serikali katika maeneo tofauti hapa nchini kufika katika banda la Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kuweza kupata elimu juu ya matumizi sahihi ya kemikali katika bidhaa zao wanazozizalisha.

Amesema matumizi holela ya kemikali yanaweza kusababisha madhara kwa mtumiaji wa bidhaa ikiwemo kuungua pamoja na kuwashwa hivyo amewataka wajasiriamali nawazalishaji wengine kuhakikisha wanatambua aina ya kemikali zinazopatikana katika malighafi wanazozitumia kabla ya kuzalisha bidhaa zao.

Pia amewataka wajasiriamali nchini kufuata kanuni za matumizi sahihi ya kemikali wanazozitumia hasa tindikali (acid ) katika kutengeneza bidhaa zao ili kuepuka madhara yanayojitokeza kutokana na matumizi holela ya kemikali hizo.

Kwa upande wao baadhi ya wananchi wa Manispaa ya Morogoro waliofika katika banda hilo wameiomba mamlaka hiyo kuendelea kutoa elimu kwa wananchi kwani wengi wao wamekuwa wakitumia kemikali mbalimbali bila ya kujua madhara yake kiafya na mazingira.

Awali mkemia mkuu wa serikali alitembea mabanda mbalimbali ya wadau pamoja na wajasiriamali wanaotengeneza bidhaa zinazotumia kemikali ambapo pamoja na mambo mengine alitumia fursa hiyo kutoa elimu ya matumizi sahihi ya kemikali. 
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...