Waziri Bashungwa ameyasema hayo katika kikao cha maafisa habari wa serikali na kuwataka kuendelea kushirikiana wadau mbalimbali wa serikali ili kuendelea kuisaidia serikali kufanikisha mipango ya maendeleo ikiwemo na zoezi la Sensa linarotajiwa kuanza rasmi mwezi wa nane mwaka huu .
Kikao hicho cha maafisa habari na mawasiliano wa Serikali kinachofanyika kila mwaka kina lengo la kukumbushana mambo mablimbali ambapo kwa mwaka huu kimefanyika kuanzia Mei 9 mpaka Mei 14 Jijini Tanga huku kikihudhuriwa na viongozi, wadau pamoja na wataalamu mbalimbali wa tasnia ya habari na mawasiliano ya Umma nchini.
Katika kikao hicho Waziri Bashungwa alikabidhi vyeti kwa wadhamini wa mkutano huo ikiwemo kampuni ya BRAVADO_GROUP iliyodhamini huduma ya upambaji, uchapishaji na sare (Branding and Printing) ambapo cheti hicho kilipokelewa na Meneja Masoko Sharifa Abdalla.
Waziri wa TAMISEMI, Innocent Bashungwa akikabidhi cheti cha udhamini kwa na Mwakilishi wa Kampuni ya BRAVADO_GROUP Sharifa Abdalla iliyodhamini huduma za upambaji, uchapishaji na sare (Branding and Printing) katika mkutano wa mwaka wa chama cha maafisa habari na uhusiano wa Serikali (TAGCO).
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...