Na Ripota  Wetu, Michuzi TV

WIZARA ya Afya imetoa maagizo kwa Taasisi ya Tiba ya Mifupa(MOI) pamoja na hospitali zote kubwa nchini kuhakikisha zinakuwa na Plani B ya kulinda mashine zote zikiwemo MRI na CT Scan kutoharibika kwa sababu mbalimbali hasa inayosababisha na kukatikakatika kwa umeme.

Maagizo hayo yametolewa leo Mei 11,2022 na Katibu Mkuu Wizara ya Afya Prof. Abel Makubi baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika taasisi ya Moi kutokana na uwepo wa taarifa za mashine za MRI na CT Scan kuharibika na kutofanya kazi kwa muda sasa.

“Tumepata taarifa kuwa kipimo cha MRI hapa MOI hakifanyi kazi na taarifa hizi tumezipata kupitia njia zetu za kupata taarifa jambo ambalo sio sawa hata kidogo. Kutokana na taarifa hizo tumeona tuje kuthibitisha ukweli wa hizi taarifa na tulipofika hapa kweli MRI haifanyi kazi lakini pia tumeambiwa na mashine ya CT Scan nayo
imeharibika.

“Habari ndio tumezipata baada ya kufika hapa, sasa kwa haya mawili tumepata changamoto kwetu sisi kama viongozi wa Wizara tumepewa sababu, tumepewa maelezo ya kwanini haya yametokea.Mashine ya MRI tumeambiwa gesi yake imepungua hivyo kushindwa kufanya kazi na CT Scan imeharibika mfumo wa umeme unatamatizo kidogo

“Tumeambiwa kuharibika huko kumechangiwa na sababu mbalimbali mojawapo ni kukatika kwa umeme , sasa sisi ni watoa huduma lakini kutokana na hayo sisi kama Wizara tunatoa maelekezo yafuatayo.Agizo la kwanza tunatoa siku 14 mashine ziwe zinafanya kazi.Kutokana na ukubwa wa hayo matatizo mliyosema nafahamu kidogo, siku 14 zinatosha,”amesema.

Pia ameagiza menejimenti ya MOI kuwa na Plan B ya kuhudumiwa wagonjwa wanaohitaji huduma kuzipata bila usumbufu wowote .“Plani B hiyo ilishaanza kufanyika ambayo ni kupata huduma kwa majirani zenu Muhimbili, hivyo muangalie namna ya kuiboresha, iwe rafiki.

“Lakini sasa kutokana na hiyo hali kwa nchi nzima naagiza vifaa vyote vyenye gharama kama ya MRI na CT Scan ambazo serikali inatumia fedha kubwa kuwekeza la kwanza waombe TANESCO kwa kushirikiana na menejimenti ya MOI kufanya tathimini ya mifumo ya umeme ya kusambaza umeme kwa vifaa hivi ambavyo ni gharama.Na hii ni kwa hospitali zote kubwa za Serikali ambazo zina vifaa vyenye gharama kubwa,”amesema.

Amefafanua tayari Wizara imeagiza CT Scan 29 kupitia fedha za UVIKO-19, hivyo mashine hizo zinaweza kuja nchini na matokeo yake zikaharibika tena.

“Muwaombe TANESCO waje hapa MOI kufanya tathimini ili kubaini nini ambacho kilisababisha hadi mashine hizi zikaharibika.Naagiza kuwepo na mfumo wa umeme ambao utasaidia kuendesha mashine hizo.Umeme unakatika unarudi unakatika unarudi, hivyo lazima tuwe na njia nyingine pale ambapo tunaona umeme umeanza kukatikakatika.

“Hili ni agizo kwa nchi zima, na hii ni kwa mashine zote ambazo gharama yake inaanzia Sh.milioni 500 , lakini vile vile agizo jingine pawepo na matengezo. Hatuwezi kuwa na mashine ambazo kila muda zinaharibika.Wanaosambaza hivi vifaa wawe wanafanya matengenezo kabla ya vifaa kuharibika.

Aidha amesema huduma zote ambazo zinaingiza mapato makubwa ikiwemo ya CT Scan, MRI na vipimo vya maabara lazima kuwe na fedha ambazo zitawekwa maalum kwa ajili ya kufanya matengenezo”Agizo hili naomba lianze kutekelezwa mara moja, Mhasibu uko hapa na umenisikia aanzeni kuweka asilimia fulani ya fedha inayotokana na vipimo hivyo na
zitengwe mahali ili mashine ikiharibika fedha inatumika kufanya matengezo,”amesema.Katibu Mkuu Wizara ya Afya Prof. Abel Makubi akitoa maelekezo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa (MOI) Dkt Respicious Boniface (wa tatu kulia) alipofanya ziara ya kushitukiza leo Mei 11,2022 jijini Dar es Salaam, kwenye taasisi hiyo kufuatia uwepo wa taarifa za mashine za MRI na CT Scan kuharibika na kutofanya kazi kwa muda. PICHA ZOTE NA MICHUZI JR-MMGKatibu Mkuu Wizara ya Afya Prof. Abel Makubi akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa (MOI) Dkt Respicious Boniface (wa pili kulia) alipofanya ziara ya kushitukiza leo Mei 11,2022 jijini Dar es Salaam, kwenye taasisi hiyo kufuatia uwepo wa taarifa za mashine za MRI na CT Scan kuharibika na kutofanya kazi kwa muda.Katibu Mkuu Wizara ya Afya Prof. Abel Makubi akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa (MOI) Dkt Respicious Boniface ndani ya chumba cha mashine ya CT Scan (wa pili ) alipofanya ziara ya kushitukiza leo Mei 11,2022 jijini Dar es Salaam, kwenye taasisi hiyo kufuatia uwepo wa taarifa za mashine za MRI na CT Scan kuharibika na kutofanya kazi .
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Prof. Abel Makubi (katikati) akizungumza mbele ya Menejimenti ya MOI mara baada kufanya ziara ya kushitukiza leo Mei 11,2022 jijini Dar es Salaam, kwenye taasisi hiyo kufuatia uwepo wa taarifa za mashine za MRI na CT Scan kuharibika na kutofanya kazi kwa muda sasa.Pichani kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa (MOI) Dkt Respicious Boniface na kulia ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Tiba (Wizara ya Afya) Dkt Omari Ubuguyu.
Baaadhi ya Menejiment ya MOI wakimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Afya Prof. Abel Makubi hayupo pichani) wakati akizungumza nao leo Mei 11,2022 mara baada kufanya ziara ya kushitukiza kwenye taasisi hiyo kufuatia uwepo wa taarifa za mashine za MRI na CT Scan kuharibika na kutofanya kazi .


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...