Na Farida Mangube,Morogoro.

Jamii imetakiwa kutunza mazingira kama hatua ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi ambayo ni hatarishi kwa Kilimo,Uvuvi na Ufugaji ili kuepukana na ugumu wa maisha kwa watu waishio vijijini.

Wito huo umetolewa na Wavuvi wa kata ya Lipangalala Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro wanaojishughulishana Uvuvi Mto Kilombero na kusema tayari wameshaathirika na madhara ya tabia nchi.

Walitaja madhara hayo kuwa ni pamoja na migogoro ya Wakulima,Wafugaji na Wavuvi katika mto huo.

Wavuvi hao tayari wamenufaika wa mradi wa Uhakika wa Maji (Fair Water Future ) wenye lengo la kutambua uwajibikaji wa viongozi wa serikali katika kutatua changamoto za upatikanaji wa maji kwa shughuli za Kilimo,Mifigo na Uvuvi.

Mmoja wa wanufaika hao ambae pia ni Shahidi wa Maji Bi. Hadija Bakari Kimwaga alisema mabadiliko ya tabianchi yamesababisha upungufu wa Samaki katika mto huo hali inayosababisha ugumu wa maisha kwa wavuvi na wachuuzi wa samaki.

Nae Bi.Mwajuma Hamadi Kikopa alisema ujio wa mradi huo umeleta manufaa makubwa kwa Wavuvi na Wachuuzi wa samaki kutokana na kuweza kutatua changamoto zao kupitia Mashahidi wa Maji.

Alisema awali walikuwa hawajui namna ya kuwasilisha changamoto zao kwa viongozi wa serikali lakini baada ya kupata mafunzo kupitia mradi wa Uhakika wa Maji na kuchaguliwa kwa Mashahidi wa Maji wameweza kuwasilisha kero zao kwenye ofisi za serikali bila ya kikwazo chochote.

Bi. Mwajuma alisema kabla ya kuanza kwa mradi huo hawakua na uelewa wa namna ya kuwasilisha changamoto zao kwa mamlaka zinazohusika mpaka kwenye mikutano ya kisiasa au inayoratibiwa na viongozi serikali.

Alisema baada ya kuanzishwa kwa mardi huo na kupatiwa elimu ya uwasilishaji wa Changamoto kwa viongozi maisha yao katika kambi za Wavuvi yamebadilika taofauti na hapo awali.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mashahidi wa Maji Bwana Andrea Justine Mtolela alisema kupitia maradi huo waliweza kuandika barua na kuorodhesha kero zao na kuziwasilisha ofisi ya Mkuu wa Wilaya Kilombero ili zifanyiwe kazi.

Aliongeza kuwa kupitia barua walioiwasilisha Mkuu wa Wilaya hiyo alifika katika kambi za wavuvi na kujionea hali halisi ya changamoto zinazowakabili wavuvi hao na kuanza kuzifanyia kazi.

Uhakika wa Maji ni maradi unaotekelezwa na Shirika lisilo la kiserikali la Shahidi wa Maji katika Wilaya mbili za Kilosa na Kilombero ukiwa na lengo la kutambua uwajibikaji wa viongozi wa serikali katika kutatua changamoto za upatikanaji wa maji na usawa wa maji kwa shughuli za Kilimo,Mifigo na Uvuvi.

Mwisho.
Mashahidi wa Maji wakiwa katika picha ya pamoja kwenye Ngalawa pembezoni mwa Mto Kilombro.
 Afisa programu wa mradi wa Uhakika wa Maji Bwana Tondole Gungulundi akizungumza na Mashahidi wa Maji wa kata mbili za Lipangalala na Sululu wilayani Kilombero Mkoa wa Morogoro.


 Mwenyekiti wa Mashahidi wa Maji katika Kata ya Lipangalala Bwana Andrea Justine Mtolela (alieshika mti) akielekeza jambo kuhusu shughuli za uvuvi katika Mto Kilombero kwa Mashahidi wa Maji kutoka kata ya Sululu waliofika kujifunza namana wavuvi walivyofanikiwa kutatua changamoto zao kupitia shahidi wa maji.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...