Na Mashaka Mhando, Muheza


WATUMISHI wilayani hapa, wamemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan, kwa hatua yake ya kuongeza mishahara kwa asilimia 23.3 kwa wafanyakazi nchini.

Sanjari na kumshukuru Rais, walisema ongezeko hilo, limekuja wakati muafaka katika kipindi ambacho dunia inapitia nyakati ngumu za kiuchumi.

Akizungumza kwa niaba ya watumishi hao, Mkuu wa wilaya ya Muheza Halima Bulembo, alisema ongezeko hilo imelenga kuongeza ufanisi wa kazi, kujituma na kupunguza makali ya maisha.

Bulembo, ambaye tangu afike Muheza mwaka jana, amekuwa akipambania maendeleo wilayani humo, alisema wamepata faraja na hivyo kuongeza imani kwa serikali yao Kwani kilikuwa ni kilio chao cha muda mrefu.

Bulembo amesema wafanyakazi wengi wamepata faraja baada ya tamko la mheshimiwa Rais na wameongeza imani na serikali yao.

"Kwa niaba ya watumishi wa Muheza tunamuombea Rais Mungu amjaalie uzima aweze kuendelea kutuongoza watanzania na kutujali Katika nyanja zote na tuahidi kuendelea kuwa na imani Nae "amesema DC Bulembo.

Mmoja wa watumishi hao Saumu Mohamed amesema wanamshukuru Rais Kwa ongezeko Hilo kwani watumishi wamefurahi Sana na kumuombea Kwa Mungu aweze kuleta mabadiliko mengi ndani ya nchi hii.

Kwa upande wake Afisa Elimu Selapyone Bashangwe amempongeza Rais kwa uamuzi wake wa kuongeza mshahara kwani umekuja wakati mwafaka

Ongezeko la mishahara limekuwa likipigiwa kelele na wafanyakazi kwa muda mrefu hasa wakati wa sherehe za wafanyakazi wakitaka serikali kuongeza kiwango cha mshahara ili kiendane na maisha halisi yaliyopo.

Mkuu wa wilaya ya Muheza, Halima Bulembo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...