
Na Khadija Kalili
MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wanawake na Watoto ya Shirikisho la Vyama Vya Watu Wenye Ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA) Nuru Awadh usiku wa juzi alitoka nje ya Ukumbi wa Mikutano wa Lion Hotel Sinza kwa kile alichodai kutoridhishwa na Mwenyekiti na Wajumbe kukubali hoja zake alizozitaka zifanyiwe kazi katika mkutano wa marekebisho ya Katiba ya Shirikisho la Vyama Vya watu wenye ulemavu SHIVYAWATA ambao ni mwamvuli uliobeba vyama kumi vya watu wenye ulemavu.
Mwenyekiti huyo alisema kuwa kuwa 'Mwenyekiti wa kikao alikuwa anapinga hoja za wanawake, kila tunavyojaribu kuchangia yeye hataki na anadai kipengele kimeshapita na haturudi nyuma, hali kadhalika wanawake walikuwa hawapewi nafasi ya kuongea hata waliponyoosha mkono juu" alisema Nuru Awadh.
"Hivyo wanawake tuliamua kutoka nje baada ya kuona katiba inayoenda kupitishwa itakuwa kandamizi kwa wanawake" alisema.
Sintofahamu hiyo ilitokea mwishoni mwa wiki katika uliohudhuriwa na viongozi 26 wa SHIVYAWATA huku wakiwakilisha Mikoa yote nchini pamoja na viongozi sita kutoka vyama 10 vya watu wenye ulemavu nchini.
Mwenyekiti huyo anamtaja Mwenyekiti wa Kamati ya marekebisho ya katiba ya kikao hicho kuwa ni Novath Rukwango.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...