- Asema kazi ya kurejebisha Miundombinu iliyoungua itafanyika usiku na mchana.
- Awahakikishia Wafanyabiashara hakuna atakaehamishwa.
- Asisitiza Masoko kuwa na Fundi umeme anaetambuliwa na TANESCO.
- Aonya tabia ya Mamalishe kuhinjika maharage jioni ili asubuhi wakute yameiva.
Na Mwandishi Wetu,Michuzi Tv
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla amesema chanzo Cha Moto uliopelekea kuteketea kwa Soko la Veterinary lililopo TAZARA Wilaya ya Temeke ilitokana na Hitilafu ya umeme.
RC Makalla amesema hayo alipotembelea Soko Hilo kujionea uharibifu wa Mali zilizoteketea moto ambapo amesema taarifa za awali zinaonyesha Moto huo umeathiri takribani vibanda 453.
Aidha RC Makalla amesema Serikali inafanya taratibu za haraka kuhakikisha kazi ya kurejesha Miundombinu iliyoharibika inafanyika usiku na mchana ili Wafanyabiashara warudi kuendelea na Biashara Kama awali ambapo ameahidi hakuna mfanyabiashara atakaeondolewa.
Hata hivyo RC Makalla ametoa pole kwa Wafanyabiashara walioathiriwa na Moto huo na kuwataka kuwa watulivu wakati Serikali yao inaendelea kutatua changamoto hiyo.
Kutokana na matukio ya Moto kujirudia Mara kwa Mara, RC Makalla ameendelea kutoa wito kwa Viongozi wa masoko kuhakikisha kila soko linakuwa na fundi umeme anaetambuliwa na TANESCO,Halmashauri kuweka Vifaa vya kudhibiti moto kwenye Kila soko, Wafanyabiashara kuacha tabia ya kuhinjika maharage jioni ili asubuhi wakute yameiva huku akisisitiza Masoko kuwa na Ulinzi.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam . Amos Makalla, akizungumza mara baada ya kufika eneo la tukio ambapo soko limeunguaMkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Amos Makalla akiawa ameongozana na Mkuu wa Wilaya ya Temeke,Jokate Mwegelo na viongozi mbalimbali eneo ambapo soko limeungua Vetenari wilayani Temeke
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla, akionyesha baadhi ya mejengo yalioanguka kutokana na moto huo
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...