Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe Anthony Mavunde amempa siku 14 mkandarasi anayetakiwa kukarabati mradi wa umwagiliaji wa Kilida uliopo katika Kijiji cha Kilida, kilichopo Jimbo la Kavuu, Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe mkoani Katavi.

Mhe Mavunde ametoa maelekezo hayo alipotembelea mradi huo kujionea uharibifu uliotokana na mvua kubwa zilizonyesha na kuharibu baadhi ya mashamba ya wakulima katika kijiji hicho.

“Nimewaelekeza Tume ya Taifa ya Umwagiliaji kuhakikisha mkandarasi anayetakiwa kujenga mradi huu awe amefika hapa ndani ya siku 14 kuanzia tarehe ya leo.

Awali mkandarasi alikuwa anasema anashindwa kuja sababu ya mvua ila nimefika mwenyewe mpaka hapa na nimejionea barabara zinapitika na hamna kisingizo nampa siku 14 aje aanze kazi tuwasaidie wananchi wetu

Tumejipanga vizuri kuhakikisha tunaongeza wigo wa kilimo cha umwagiliaji hapa chini ili kufikia malengo tuliyojiwekea ya kukuza sekta ya kilimo kwa asilimia 10 ifikapo mwaka 2030.

Maeneo ambayo Mh Rais Samia Suluhu Hassan ameelekeza tuyape msisitizo ni kilimo cha umwagiliaji,na ndio maana nipo hapa kuhakikisha skimi hii inafanya kazi kwa ukamilifu ili wananchi wengi wanufaike”Alisema Mhe Mavunde.

Awali Mbunge wa Jimbo la Kavuu na Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe Geophrey Pinda amesema kuwa mradi huo wa umwagiliaji utakapojengwa na kukamilika licha tuu ya kutoa ajira utasaidia pia kuzalisha mbegu.

“Tunataka hapa pawe na mradi mkubwa wa umwagiliaji utakaosaidia uzalishaji mkubwa wa mbegu. Wananchi wa huku wanaumizwa sana na bei ya mbegu ila zikizalishwa hapa maisha ya wananchi wengi hapa yatabadilika,” amesema Mhe. Mbunge huyo.











 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...