Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, ameitisha Kikao cha dharura usiku wa leo tarehe 08 Mei Ikulu ya Dar es Salaam kujadili tatizo la kupanda kwa bei ya mafuta nchini.

Miongoni mwa waliohudhuria kikao hicho ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Waziri wa Nishati January Makamba, Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato ya Tanzania (TRA) Alphayo Kidata na makatibu wakuu wao.

Katika kikao hicho, Rais Samia amewaagiza viongozi hao kutafuta suluhisho la haraka katika kukabiliana na tatizo hilo la Upandaji wa bei ya Mafuta nchini


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...