Naibu Waziri wa Kilimo, Mh. Antony Mavunde ameeleza kwamba Serikali kupitia wizara ya Kilimo imeweka mpango madhubuti wa kuongeza ushirikishwaji wa vijana kwenye shughuli za kilimo nchini kwa kuanza utekelezaji wa programu ya Toboa na Kilimo (BBT) ambapo jumla ya ekari 20,000 zimetengwa katika wilaya za Chamwino na Bahi mkoani Dodoma kama eneo la majaribio.
Naibu Waziri Mavunde ameyasema hayo leo tarehe 31 Mei, 2022 wakati akizindua rasmi kitabu chenye hamasa kwa vijana kuhusu mafaniko yao binafsi kwenye Sekta ya Kilimo kupitia Mradi wa Kuwaendeleza Vijana kwenye Kilimo (Advancing Youth Impact) uliotekelezwa kupitia Mradi Mkubwa wa Feed the Future unaosimamiwa na Shirika la Maendeleo la Marekani USAID hafla iliyoenda sambamba na makabadhiano ya magari mawili yaliyotolewa kwa Wizara ya Kilimo kwa ajili ya kutekeleza programu za vijana za Kilimo.
"Kwa mujibu wa Utafiti wa Watu wenye Uwezo wa Kufanya Kazi uliofanywa na NBS, vijana wanajumuisha zaidi ya asilimia 60 ya nguvu kazi ya Taifa letu, hivyo tukiwashirikisha vijana kwenye sekta za uzalishaji hakika tutafikia malengo yetu haraka na kwa ufanisi mkubwa.
Wizara ya Kilimo kupitia bajeti ya mwaka ujao wa fedha, itatekeleza Programu ya vijana itakayoitwa **Building today for a Better Tommorow **yenye lengo la kuwapatia vijana mashamba ambayo yatakiwa yamewekewa miundombinu yote, ikiwa ni pamoja na kuungaishwa na masoko. Lengo ikiwa ni kuongeza ushiriki wa vijana kwenye kilimo na kupunguza tatizo la ajira kwa vijana na kuongeza upatikanaji wa chakula na mazao ya kimkakati ikiwemo alizeti.
Kama sehemu ya utekelezaji wa programu ya BBT, Mkoa wa Dodoma umetenga eneo la ekari 20000 ambalo kwa kuanzia vijana watapangwa vizuri na kupata mahitaji yote stahiki na muhimu ili walime alizeti kama sehemu ya mkakati wa kupunguza uagizaji wa mafuta ya kula kutoka nje ya nchi.
Nawapongeza sana Shirika la USAID kwa kuja na aina hiyo ya Mradi ambao Umelenga kuleta athari chanya za maendeleo kwa Vijana wa Tanzania Bara na Tanzania Visiwani (Zanzibar) na kwa niaba ya serikali ninawashukuru sana kwa magari haya mawili ambayo yatatumika kutekeleza mradi wa Vijana”Alisema Mavunde
Naye Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Marekani nchini Tanzania (USAID) **Bi. Kate Somvongsiri **amsema kwamba USAID itaendelea kushirikiana na Serikali kuwezesha vijana wengi zaidi katika kujishughulisha na kilimo na kwamba wapo tayari kushirikiana na serikali kuona vijana wengi zaidi wanashiriki kwenye sekta hii ya kilimo na kwa kuanzia katika kutekeleza mradi huo wametoa magari mawili aina ya Toyota Land Cruiser 76 Hardtop kwa ajili ya kufanikisha utekelezaji wa mradi huu
Home
KILIMO
PROGRAMU YA VIJANA YA TOBOA NA KILIMO (BBT) KUANZA NA ENEO LA EKARI 20,000 MKOANI DODOMA.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...