NA MWANDISHI WETU, TANGA

MFUKO wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) unashiriki katika maonesho ya bishara na utalii kwa kutoa elimu kwa wanachama kupitia maonesho yanayofanyika katika viwanja vya Mwahako jijini Tanga.

PSSSF inashiriki katika maonesho haya pamoja na kutoa elimu kwa wanachama na wananchi wanaotembelea banda hilo, pia wanachama wanapatiwa huduma mbalimbali za kiofisi ikiwemo, kuangalia taarifa za michango ya wanachama, taarifa za malipo ya pensheni, uhakiki wa wanachama na kutoa ufafanuzi kuhusu masuala mbalimbali ya uanachama, alisema Bi. Rehema Mkamba, Afisa Mkuu wa Uhusiano, PSSSF

Alisema ni fursa nzuri kwa Mfuko kukutana na wanachama wake lakini wananchi pia ambao watafika kwenye maonesho hayo maarufu kama Tanga Trade Fair ambayo yatadumu kwa siku 10 kuanzia Mei 28 hadi Juni 6, 2022.
Wanachama wa PSSSF wakihidumiwa kwenye banda la Mfuko huo kwenye Maonesho ya biashara na utalii kwenye viwanja vya Mwahako jijini Tanga.
Wananchi na wanachma waliofika kwenye banda la PSSSF weakijisajili kwenye kitabu cha wageni baada ya kuhudumiwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...