Na Said Mwishehe,Michuzi TV

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewashuku watanzania wote ambao wamefanikisha kukamilika kwa uaandaji wa filamu ya Royal Tour ambayo inakwenda kuutangaza utalii uliopo nchini.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa filamu hiyo uliofanyika leo Mei 8,2022 jijini Dar es Salaam Rais Samia pamoja na mambo mengine ameelezea kufurahishwa kwake na ushiriki wa Watanzania hadi kufanikisha kukamilika kwake.

“Kazi mtakayoina kwenye filamu ya Royal Tour haikuwa rahisi na hapa tulikofikia tumejitahdii kweli kweli, nawashukuru viongozi wote wa Serikali, Bunge, Mahakama, Chama Cha Mapinduzi, wasanii na watanzania wote.

“Kuna wengi ambao wamejitokeza moja kwa moja na wengine walijitolea chakula, mafuta na wapo walituwezesha katika malazi kama sehemu za kulala.Nawashukru wadau wote ambao wamejitolea kufanikisha filamu hiyo kutoka sekta ya utalii

“Natoa salamu za kipekee kwa Rais wa wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dk.Hussein Mwinyi na nampongeza kwa kwa kufanikisha uzinduzi wa filamu hii kule Zanzibar,”amesema Rais Samia alipokuwa akitoa shukrani zake kwa wote walioshiriki kufanikisha filamu hiyo.

Aidha Rais Samia amempongeza mtayarishaji wa filamu hiyo Peter Greenberg kwa kazi kubwa ambayo ameifanya, lakini tunaipongeza Kamati maalum yenye watalaam wa ndani.

“Kazi hii ilianza kama wazo kutoka kwa watanzania Diaspora walioko nchini Marekani na kisha wakazungumza na kampuni ambayo imetengeneza filamu hii.Hata hivyo kabla ya kutengeneza filamu hiyo nilikutana na mabaraza mbalimbali.

“Juni mwaka jana tulikaa na Baraza la Biashara na kuwaomba waniunge mkono, Agosti mwaka jana niliandaa chakula cha hisani ili kupata michango.Lengo lilikuwa kupata Sh.bilioni 20 lakini ahadi zilipatikana Sh.bilioni19.5 na makusanyo ya fedha yalikuwa Sh.bilioni 12.7

“Sekta zilizochangia ni Uwekezaji, Uzalishaji na Biashara, pia sekta ya fedha na utalii,na kulikuwa na kamati maalum ya kuhamasisha michango,”amesema Rais Samia .

Amefafanua matumizi ya fedha hizo ni kuwa fedha yote iliyokusanywa ndio iliyotumika kwenye Royal Tour ambapo Sh.bilioni saba zimetumika na nyingine ilitumiwa na Kamati kufanya safari za kwenda na kurudi.

“Fedha iliyobakia itatumika kutengeza awamu ya pili na awamu ya tatu ya Royal Tour kwani picha zilichukuliwa nyingi.Wakati sisi tuko hapa Dar es Salaam kwenye uzinduzi huu kuna watanzania wamefunga screen zao na wanafuatilia,”amesema.

Kuhusu changamoto ambazo amekutana nazo wakati wa kuandaa filamu hiyo ni pamoja na kuacha ofisi kwa siku 8 kwenda kutengeneza sinema.“Ilikuwa changamoto kubwa.

“Ni kazi ambayo kwangu ni ngeni hivyo ilikuwa ngumu kurekodi, kuna wakati nilikuwa narudia zaidi ya mara moja.Changamoto nyingine ni usalama kwani kuna wakati walikuwa wanazuia…Usifanye.

“Hivyo leo tunahitimisha kitaifa kuizindua filamu ya Royal Tour kwani tulianza Marekani, kisha Arusha, Zanzibar na sasa Dar es salaam. Kuanzia sasa filamu hii itakuwa ikioneshwa na maeneo yote ili watanzania waione,”amesema Rais Samia.

Akieleza zaidi amesema filamu hiyo ni kwa ajili ya kizazi cha sasa na kijacho na imefungua milango ya Tanzania katika nyanja mbalimbali ikiwemo sekta ya utalii.

“Sekta ya utalii iko laini sana inapanda na kushuka, hivyo tumeona tuipe nguvu.Wakati wa janga la Covid-19 utalii ulishuka na watanzania wengi walipoteza ajira.Wote tunajua Arusha na Zanzibar inategemea utalii na hata utalii ukiwa chini unaona mambo yalivyokuwa.

Aidha amesema wakati wa Covid watalii na mapato yatoyokanayo na utalii yalishuka. “Walioathrika zaidi ni waongoza watalii, wenye hoteli, wabebaji watalalii , hivyo kutokana na athari hizo wameona ni vema kuutangaza utalii kupitia fimu hiyo.

“Filamu ilikamilika Machi mwaka huu 2022 na kuanzi mwezi huo vilianza kurushwa vipande vipande ambavyo vimesaidia kuongeza idadi ya watalii pamoja na pato la taifa ambalo limeongezeka kwa asilimia asilimia 48.6

Rais Samia amesema watalii kutoka nje ya Tanzania wamekuja nchini kwa ajili ya kuona vivutio vya utalii na kuongeza filamu hiyo imeonesha hali ya mazingira ya Tanzania na tayari wamepokea maombi kwa kampuni ambazo zinazohitaji Kaboni baada ya kuona msitu uliko nchini.

“Nimeamua niseme hayo madogo ambayo yameanza kuonesha matumaini kutokana na filamu,”amesema Rais Samia alipokuwa akielezea mafanikio ambayo yameanza kuonekana baada ya kuzinduliwa kwa filamu hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...