RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Viongozi wa Serikali na Dini baada ya kuwasili katika Masjid Jamiu Zinjibar Mazizini Unguja kuhudhuria Sala ya Eid Fitry baada ya kumalizika kwa Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, Sala hiyo iliyofanyika katika Masjid hiyo leo 3-4-2022.



RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akijumuika na Waumini wa Dini ya Kiislam katika Sala ya Eid Fitry iliyofanyika leo asubuhi katika Masjid Jamiu Zinjibar Mazizini Unguja Jijini Zanzibar, baada ya kumalizika kwa mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani, (kulia kwa Rais) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba,Sheria,Utumishi na Utwala Bora Mhe. Haroun Ali Suleiman, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe.Othman Masoud Othman, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla, Makamu wa Rais Mstaafu Mhe. Mohammed Gharib Bilal na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Zuberi Ali Maulid.



RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa katika viwanja vya Masjid Jamiu Zinjibar Mazizini Unguja wakati ikipingwa mizinga baada ya kumalizika kwa Sala ya Eid Fitry iliyofanyika katika Masjid hiyo na (kulia kwa Rais) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba,Sheria, Utumishi na Utawala Bora Mhe.Haroun Ali Suleiman na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Idrisa Mustafa Kitwana na (kushoto kwa Rais) Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla.(Picha na Ikulu)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...