Na Said Mwishehe, Michuzi TV –Lindi

MKUU wa Mkoa wa Lindi Zainab Tarik amemwambia Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Shaka Hamdu Shaka kwamba umefika wakati jamii ya Watanzania kuambiwa ukweli kuhusu mkoa huo siio masikini kwani una kila kitu ambacho kinapatikana Duniani.

Akizungumza mbele ya Shaka pamoja na wananchi wa Kijiji cha Kalangala A ,Mkuu huyo wa Mkoa wa Lindi amesema katika mkoa wa Lindi kuna bahari ya Hindi, mazao ya kimkakati ambayo ni ya kimataifa kama korosho na ufuta pamoja na madini ya aina zote ukiondoa Almasi na Tanzanite.

"Kwa mfano korosho peke yake tunapata kuanzia Sh. Bilioni 129 mpaka Sh. bilioni 150 kwa mwaka, ufuta tunapata kuanzia Sh.bilioni 121 mpaka Sh.bilioni 126 kwa mwaka. Lindi ndio mkoa pekee ambao una madini yote yanayopatikana duniani ukiacha Almasi na Tanzanite madini mengine yote tunayo.

“Tuna madini amabyo sasa hivi yanatafutwa duniani, 'Mangannese na Graphite' kila unakokanyaga kwenye mkoa wetu wa Lindi madini hayo yapo, lakini tuna madini ya kutengeneza simenti, jasi inayopatikana katika Mkoa wa Lindi peke yake na Manyara na Singida kidogo, lakini madini yanayopatikana Lindi ni namba moja,”amesema.

Ameongeza kwamba viwanda vyote vya saruji vinategemea madini hayo kutoka Lindi. Kwa hiyo watu wanapoiangalia Lindi naomba waiangakie kwa jicho la pekee, ni Mkoa ambao wafanyabiasha wote wanatakiwa kukimbilia.

“Tumsaidie Rais wetu katika kutengeneza uchumi wa wanalindi kwa malighafi ambazo ziko Lindi.Tunamshukuru Rais anatutengenezea bandari ya kisiasa ya Uvuvi pale Kilwa, tayari amemwaga fedha kwa ajili ya ujenzi huo,”amefafanua.

Mkuu huyo wa Mkoa amesema katika miaka yote bandari ya Kilwa imekuwepo na hakuna aliyeitengeneza lakini katika kipindi hiki cha utawala wa Rais Samia inakwenda kujengwa.“Lakini ni wakati huu wa mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan anasema Soko la kosho duniani ni kubwa sana na ndiomana na sisi tunahamasisha mashamba mapya na tunahamasisha kuondoa mashambapori.”



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...