Na Said Mwishehe,Michuzi TV -Lindi

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kupitia kwa Katibu wake wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka, kimesema umefika wakati kwa wananchi kuungana na Rais Samia Suluhu Hassan kupiga vita matendo yote yanayodhalilisha na kukatisha mdoto za mtoto wa kike kupata elimu.

Shaka amesema hayo leo Mei 30 mwaka 2022 baada ya kutembelea na kushiriki ujenzi wa shule maalumu ya Wasichana ya Mkoa wa Lindi inayojengwa katika Kijiji chaKilangala B mkoani Lindi.

Amesisitiza kuwa ipo haja ya kumuunga mkono kwa vitendo Rais Samia Suluhu Hassan ambaye amejipambanua katika kuleta usawa kijinsia kuanzia ngazi ya chini na kupiga vita udhalikishaji.

Shaka amesema Rais Samia tangu ameingia madarakani amekuwa kinara wa usawa wa kijinsia nchini na amekuwa akichukua hatua mbalimbali za kuhakikisha usawa unakuwepo. “Tangu ameingia madarakani moja ya jambo ambalo amejipambanua nalo ni uswa wa kijinsia, lakini ametoa kipaumbele kwenye jambo hili.

"Amekuwa na msisitizo sana kuwasaidia watoto wa kike sio kwamba anabagua wengine hapana, anao msukumo kwa sababu huko tulikotoka hali haikuwa nzuri katika mtazamo wa kumtunza na kumlinda mtoto wa kike,”amesema Shaka.

Hivyo amesema umefika wakati suala la usawa wa kijinsia linazungumzwa sio mdomoni tu bali kwa vitendo kuanzia ngazi ya Mkoa, Wilaya,Kata ,Vijiji na Vitongoji.“Tuhakikishe kwamba usawa wa kijinsia unapewa nafasi yake, na hii yote ni kuleta ukombozi ndani ya taifa letu.”

Amefafanua nchi yetu imepata kiongozi ambaye ameonyesha utayari wake katika kumkomboa mtoto wa kike, na kuonyesha utayari katika kusimamia na kuhakikisha usawa wa kijinsia."Walio wengi wanaweza kutafsiri usawa huu wa kijinsia unaishia kwenye kuteuana tu, hapana, hatugusi kwenye kuteuana tu.

“Kwenye kuteuana tunateuana, lakini lazima tuunge nguvu za pamoja wazazi, walezi wakinababa na wakinamama. Tunapiga vita mambo yote yanayomdhalilisha mtoto wa kike, lakini mambo yote yanayowadhalilisha watoto wetu.”

Aidha amesema anatoa pongezi kwa viongozi wa Mkoa wa Serikali ya Mkoa wa Lindi pamoja na viongozi wa CCM kwa kuunga mkono jitihada za Serikali Kuu kwa namna wanavyosimamia utekelezaji wa sera, mipango na utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ambapo kuna mambo kadhaa yaliahidiwa kwa kipindi cha miaka mitano ikiwemo kubadilisha sekta ya elimu.

Amesema Lindi ni moja ya mikoa ambayo imekuwa na mfumo dume kwa muda mrefu ambao hausaidii kwenye kusukuma na kuharakisha maendeleo ya taifa.

"Kwa hiyo mkuu wa Mkoa, Chama na wananchi wote tuna kazi ya kufanya kumuunga mkono Rais Samia kwa kufanya mabadiliko kwenye mkoa huu ili wote tuimbe ama wote tuende na kauli moja ya kumsaidia ama kumkomboa mto wa kike katika Mkoa wa Lindi,”amesema.

Ameongeza mkoa huo ni miongoni mwa mikoa inayoongoza kwa mimba za utotoni.“Tujiulize shida ni nini? Mkoa huu wasichana wengi wamekatishwa masomo yao, wamekosa fursa muhimu, ni Mkoa ambao wasichana wameathirika kisaikolojia kutokana na vitendo viovu na mambo kadhaa ambayo wanafanyiwa kinyume na ubanadamu.

"Jambo la kufurahisha Rais Samia Suluhu Hassan ameonesha utayari wake wa kumkomboa mtoto wa kike, lakini ameonyesha utayari wake katika kusimamia na kuhakikisha usawa huu wa kijinsia maana walio wengi wanaweza kutafsiri usawa huu wa kijinsia unaishia kwenye kuteuana tu, hapana, hatugusi kwenye kuteuana tu.

“Kwenye kuteuana tunateuana lakini ni vema tuunganishe nguvu za pamoja kuanzia wazazi, walezi na wananchi kupiga vita mambo yote yanayomdhalilisha mtoto wa kike,”amesema Shaka na kusisitiza kuwa Serikali ya Awamu ya Sita imetoa fedha nyingi kwa ajili ya sekta ya elimu pamoja na sekta nyingine za maendeleo.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...