Na Pamela Mollel,Arusha .
SERIKALI imejipanga kuendelea kufanya maboresho katika ofisi ya wakili mkuu wa serikali ili kuiwezesha ofisi hiyo kumudu kusimamia vyema uandaaji wa nyaraka za kesi mbalimbali za ndani na nje ya nchi kwa wakati.
Hayo yamebainishwa leo jijini Arusha na katibu mkuu wizara ya sheria na katiba Mary Makondo wakati akifungua rasmi mafunzo ya siku tano kwa mawakili kutoka wizara zote 24 za serikali na mawakili kutoka taasisi Zaidi ya 90 za serikali na binafsi .
Mafunzo hayo maalumu yameandaliwa na ofisi ya wakili mkuu wa serikali kwa mawakili hao kuwaongezea ujuzi katika usimamizi wa mashauri mbalimbali yanayoihusisha serikali ama taasisi za serikali ndani na je ya nchi dhidi ya kampuni binafsi na pia kuwa na weledi katika kutafsiri hukumu zinazotolewa nje ya nchi dhidi ya serikali ya Tanzania.
Akizungumza wakati wa ufunguzi huo katibu Makondo alisema anaelewa majukumu mazito waliyonayo mawakili wa serikali na wao kama wizara wanawajibu wa kuwasaidia kutimiza majukumu hayo kwa kuwawezesha katika Nyanja za mafunzo na vitendea kazi ili kufikia malengo.
Aidha lisema kwa kutambua changamoto mbalimbali walizonazo hususani za upungufu wa watumishi katika ofisi hiyo hususani wataalam katika sekta za mafuta gesi na madini wapo katika hatua mbalimbali za maandiko ya miradi ili kupata fedha kutoka kwa wahisani kuwezesha kusomesha wataalam wa fani hizo nje ya nchi kwa lengo la kuongeza weledi katika ofisi hiyo.
Awali akiongea kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi wakaili mkuu wa serikali Gabriel Malata aliongelea mafanikio makubwa waliyoyapata ofisi hiyo toka kurejeshwa rasmi miaka mitatu iliyopita kwa kufanikisha udhibiti na urejeshwaji wa fedha za serikali takribani tirioni 10 mpaka sasa.
Aidha alisema fedha hizo zilipatikana kutokana na usimamizi bora katika mashauri mbalimbali yaliyosimamiwa na ofisi yake katika kesi za ndani ya nchi na malipo mbalimbali yasiyostahili yaliyotaka kufanywa na taasisi za serikali.
Pia alisema licha ya mafanikio hayo wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya upungufu wa watumishi ambapo alisema ofisi hiyo inahitajika kuwa na watumishi 372 lakini mpaka sasa inawatumishi 174 pekee.
Alisema katika mkakati wa ofisi kuziba upungufu wa baadhi ya watumishi muhimu katika ofisi yake ndio maana wanalazimika kuwa na mafunzo makhsusi kama hayo kuwajengea uwezi watumishi ili kuwawezesha kutimiza majukumu yao kwa weledi katika mashauri yote watakayokabiliana nayo.
Alisema kwa kulitambua hilo ndio maana wamelazimika kutumia wakufunzi wabobezi katika mafunzo hayo ambao miongoni mwao ni majaji akiwemo jaji mstaafu Robert Makaramba, Gavana wa benki kuu Prof. Florensi Luoga, Zahra Mruma jaji wa mahakama kuu ya Tanzania na jaji mfawidhi wa mahakama kuu kanda ya Morogoro na jaji Paulo Ngwembe.
Mafunzo hayo ya siku tano yanahusisha mawakili wa serikali Zaidi ya 600 kutoka taasisi zote za serikali pia ikihusisha mawakili kutoka katika mhimili wa Bunge , Mhakama na ofisi ya msajili wa vyama vya siasa.
Katibu mkuu wizara ya Katiba na sheria Mary Makondo akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo ya mawakili wa Serikali yalionza rasmi Mei 23,2022 jijini ArushaSehemu ya Mawakili wa Serikali wakifuatilia mafunzo
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...