Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
KAMPUNI ya Michezo ya Kubashiri ya Sportpesa imeendelea kuboresha huduma zake kwa kuzindua Supa Jackpot ya Bilioni Moja (Tsh. 1,000,000,000) ambapo mchezaji wa atabashiri na kushinda kiasi hicho cha fedha kwa kuweka kiasi cha Shilingi Elfu moja (Tsh. 1,000).

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Tarimba Abbas amesema Supa Jackpot itakuwa na jumla ya michezo 17 na pia kiwango cha Pesa ambacho mchezaji atatakiwa kuweka ni Tsh. 1,000 ili aweze kucheza Jackpot hiyo.

Tarimba amesema Jackpot hiyo imegawanyika katika makundi, vipengele vitano vya zawadi ambavyo vyote mchezaji anachaguo la kushiriki na kushinda Jackpot hiyo.

“Kipengele Namba moja ni timu 17 ambapo ukishinda unaondoka na kuanzia Bilioni 1 kutengemeana na Jackpot imesimama kiasi gani. Kipengele hiki Bonasi zake zinaanzia timu 16 mpaka 12, ukipata timu 16 ukipata Bonasi la Shilingi Milioni 750, ukibashiri na ukapata michezo 15 utapata Bonasi la Shilingi Milioni 500, ukibashiri na kupata michezo 14 utapata Shilingi Milioni 300 na ukipata michezo 13 utapata Bonasi la Milioni 200”, amesema Tarimba.

Pia, amesema katika Jackpot hii ya Mechi 17 Mchezaji anaweza kuweka kombinesheni 10 ambazo ni dabo tofauti na zamani ulikuwa unaweza kuweka kombinesheni 7 pekee. Amesema hadi sasa kutakuwa na Jackpot mbili kila wiki ambayo ni zaidi ya Milioni 200.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Tarimba Abbas (Kushoto) akitoa maelekezo kwa Waandishi wa Habari namna ya kubashiri Supa Jackpot yenye michezo 17, wa kulia ni Meneja wa Uhusiano na Mawasiliano wa Sportpesa, Sabrina Msuya.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...