Kwa Upande wake Waziri wa Habari Mawasiliano na Teknolojia ya habari Nape Nauye Amesema kuwa wahabari wanao Wajibu wa kukabiliana na changamoto zilizopo na kulisaidia Bara la Afrika na kuhakikisha rasilimali zilizopo zigeuke kuwa baraka na siyo mafarajano,ili lifaidike na wananchi wao wajivunie kuwa kwenye Bara lao.
"Ukilingamisha rasilimali zilizopo Afrika na sisi tulivyo hatupaswi kuwa Kama tulivyo Sasa ifike wakati waandishi wa habari mtutumie kalamu zenu vyema kuisaidia Jamii kuziona fursa zilizopo"alisema Nape
Amesema kutokana na mada mbalimbali zitakazojadiliwa katika kongamano hilo la Uhuru wa Vyombo vya habari, watumie msingi katika kuendeleza,shughuli za wanahabari katika kupata Elimu mbalimbali ikiwemo wa sheria,sheria ya kupata taarifa pamoja na kanuni zake 2016,itasaidie kupata uzoefu utakaosaidia mchakato wa mapiitio ya sheria hiyo
Amewataka washiriki kujadiki kwa kina changamoto zinazowakabili sekta ya habari Barani Afrika,ulinzi na Usalama wa waandishi wa habari, ili waone ni namna gani wanaweza kuzitatua katika nyakati hizi za ukuaji wa teknolojia za habari
Kwa Upande wa Balozi wa EU nchini Tanzania Manfredo Fanti amesema kuwa Kuhakikisha kuwa Kuna uhuru na Usalama ka waandishi wa habari ni changamoto ya dunia ,kwani zaidi ya mashambulizi ya kidigitali 439 yamefanywa kwa waandishi wa habari, yameleta changamoto na wengine kuwashambuliwa kwa maneno na kuweka hatarini.
Akitolea mfano wa vita inayoendelea nchini Ukren amese kuwa habari za uongo zinatumika na kupunguza kutambulika kwa tasnia ya uwaandishi wa habari , hivyo Umoja wa Ulaya unaandaa sheria ya kulinda uhuru wa vyombo vya habarinkama vile ambavyo mwaka 2021,ambapo umoja huo ulileta sheria ya kuilinda waandishi wahabari
Amezitaka Taasisi mbalimbali kuwasaidia waandishi wa habari kuwasaidia waandishi pale akaunti zao zinapoingiwa na uhalifu wa kimtandao ,pamoja na changamoto za Kijiditi katika nchi za Ulaya ambapo umoja huo unatekeleza mikakati mbali katika hilo haswa uhuru wa vyombo vya habari na uhuru wa kujieleza na kulinda haki za binadamu
" Hadi Sasa tumeweza kuwasaidia waandishi 550 Ulimwengu kote kutokana na program mbalimbali tulizoziweka"
Mkuu wa Mawasiliano Win Mussabayana kutoka Umoja wa AFRIKA amesisitiza kuwa ,umoja huo unamamlaka katika nchi 55 Barani katika kuhakikisha Kuna Maendeleo na utengamano Barani Afrika na kuhakikisha ipo katika ngazi za dunia
Amesema Afrika inatakiwa kuondokana na dhana ya zamani inayoonejana kuwa afarika ni Bara la magonjwa ,rushwa na umasikini hivyo wanahabari
wanayo nafasi kwaajili ya kusimamia hilo na kubadilisha dhana hiyo kwenye agenda ifikapo 2063 kuelezwa mtazamo mpya wa AFRIKA
Mkurugenzi wa UNESCO Kanda Afrika Mashariki Prof.Hubert Gjzen amesema kuwa ni Furaha yake kubwa kujumuika na wanahabari siku ya leo katika siku ya uhuru wa vyombo vya habari na kusema.kuwa siku hii ni muhimu kwa Bara lote la Afrika
Amesema.Tanzania imeondoa vikwazo vya vyombo vya habari 4 na kurahisisha upatikanaji wa habari na kulinda uhuru na Hali ya msingi Kama ilivyoainishwa kwenye Maendeleo endelevu no 16
1945 UNESCO imekuwa mpiganaji mkubwa wa Haki za binadamu ambapo 1991 ulianzishwa mapambano Dhidi ya uhuru wa vyombo vya habari Windsock Namibia huru wa vyombo ambapo Sasa umri wa miaka 30
"Nimesikitishwa Sana wakati wa kanga la COVID 19 habari nyingi zilikuwa za uongo na uzushi haswa kwenye majukwaa ya kidigiti na tunathubutu kusema kuwa tasnia imeingiliwa hivyo tunahitaji kusisitiza jukumu la vyombo vya habari ili kulinda faragha za watu" alisema
Kwa mwaka 2021 washiriki wa uhuru wa vyombo vya habari walipitisha azimiao la windowck kwmaba Tunatakiwa kulinda Usalama wa waandishi wa habari mahali pa kazi nankuzingatia changamoto mpya zinazoletwa na teknolojia.
Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Jukwaa la wahariri nchini Tanzania Deodatus Balile amesema kwa Mara ya kwanza, shughuli hiyo ya uhuru wa vyombo vya habari kutoka nchi 54 Barani Afrika na wageni wasiopungua 100 ambapo siku ya kwanza zaidi ya 280.
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye akizungumza wakati akifungua maonesho
mbalimbali kuelekea maadhimisho ya siku ya Uhuru wa vyombo vya Habari Duniani
yatakayofanyika Mei 3,2022 jijini Arusha.
Katibu Mkuu
wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Jim Yonazi akizungumza wakati wa ufunguzi wa maonesho mbalimbali kuelekea
maadhimisho ya siku ya Uhuru wa vyombo vya Habari Duniani yatakayofanyika Mei 3,2022
jijini Arusha.
Mwenyekiti wa Jukwaa la
Wahariri nchini (TEF), Deodatus Balile, akizungumza wakati
wa ufunguzi wa maonesho mbalimbali kuelekea maadhimisho ya siku ya Uhuru wa
vyombo vya Habari Duniani yatakayofanyika Mei 3,2022 jijini Arusha.
Mkurugenzi wa Mawasilianon
wa Tume ya Muungano wa Umoja wa Afrika, Musabayana Wynne Zvinaiye akizungumza wakati
wa ufunguzi wa maonesho mbalimbali kuelekea maadhimisho ya siku ya Uhuru wa
vyombo vya Habari Duniani yatakayofanyika Mei 3,2022 jijini Arusha.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...