Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha
MKOA
wa Pwani umejipanga Kuwa ukanda wa Viwanda , Uwekezaji na mkoa wa
kimkakati, Kutokana na Hilo Taasisi wezeshi za Serikali , Halmashauri
zimeaswa kuondoa ukiritimba kwenye utoaji vibali na kutokuwa sehemu ya
kukwamisha juhudi za kukuza sekta ya uwekezaji.
Aidha Taasisi hizo ,zimeagizwa kuhakikisha zinafika katika maeneo ya Kongani za uwekezaji kutoa msaada pale inapotakiwa.
Akitembelea
baadhi ya Kongani za uwekezaji wa Viwanda ikiwemo Kampuni ya SINOTAN
(Kibaha Industrial Park Ltd ) , kujionea maandalizi ya miradi ,Mkuu wa
mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge alisema hatokubali kuona Taasisi ambayo
itaweka urasimu ili kudidimiza juhudi zinazofanywa na mkoa na Taifa
kijumla.
Alifafanua, Eneo
la Sinotan lipo Kwala linatarajiwa Kuwa kubwa katika BARA LA AFRIKA
,lina ukubwa wa heka 2,500 na walishakabidhiwa miezi miwili iliyopita na
litajengwa viwanda zaidi ya 200.
"Tunaona
namna gani Rais Samia Suluhu Hassan anavyopambana kuinua sekta ya
uwekezaji na kuitangaza nchi ili kuvutia wawekezaji ,niahidi mkoa wa
Pwani utakuwa nyuma yake kusimamia kongani hizi na kuboresha miundombinu
ya uwekezaji"
Kunenge
aliwakaribisha wawekezaji Duniani ,waje kuwekeza Mkoani hapo kwani Ni
eneo salama kwa uwekezaji, Mazingira Bora na Ni mkoa wa kimkakati.
Nae
Mkurugenzi wa Kampuni nyingine ya Uwekezaji Yusuph Manzi alieleza ,
maandalizi yanakwenda vizuri ambapo awamu ya kwanza itamamilika mwezi wa
kumi na baada ya hapo wataanza awamu ya pili .
Manzi alisema, matarajio yao ni kuwa eneo kubwa la uwekezaji ambalo litaleta tija kwenye Pato la Taifa na kuongeza ajira .
Kwa
upande wake, Mkuu wa wilaya ya Kibaha Sara Msafiri, alisema Kibaha
imetenga maeneo ya uwekezaji na kwasasa wanahakikisha wanasimamia
mipango ya Halmashauri na kuzisimamia Taasisi zote ili kuondoa vikwazo
vitakavyorudisha nyuma juhudi za Serikali.
Licha
ya mkoa huo kusheheni viwanda kila wilaya ,kwasasa Lina Jumla ya
kongani 23 za uwekezaji ambazo zinazotarajia kuinua maendeleo na uchumi
wa mkoa na Taifa na kupunguza mkali ya ukosaji wa ajira .
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...